{"id":924463,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/924463/?format=json","text_counter":340,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":"Bw. Spika wa Muda, umetoa uamuzi hapa ukasema ya kwamba sheria iko wazi kabisa kwamba ikiwa wakati wa kupiga kura, kila mtu aketi pale alipo; asitembee. Lakini sijui kama macho yangu yameona makengeza kwa sababu Sen. Linturi wa Meru alikua anatembeatembea hapa ndani. Sasa sijui kama umeona ama hukuona. Hiyo ni sawa?"}