{"id":953985,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/953985/?format=json","text_counter":95,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Bw. Spika, kuna mambo ambayo lazima mahakama ifuatilie. Hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayolinda haki za Wakenya ilihali wale wanaotakikana kulinda hizo haki wanazikanyaga na kuendelea kunyanyasa Wakenya wasio na hatia."}