{"id":954227,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/954227/?format=json","text_counter":337,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Bw. Spika wa Muda, nimetangulia kusema kwamba miundo msingi ni duni katika nchi yetu ya Kenya. Barabara zinazoelekea katika maeneo ya utalii zinaoshwa na mvua na hazipitiki."}