{"id":959580,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/959580/?format=json","text_counter":350,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Tumeona katika miji kama vile Mombasa kuwa hakuna misitu mikubwa isipokuwa ile ya mikoko yaani Mangrove forests . Hii pia imeingiliwa na kukatwa kiholela kwa sababu ya changamoto ya sehemu ya kuishi na miti ambayo inatumika kama kuni na katika ujenzi wa nyumba."}