{"id":965145,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/965145/?format=json","text_counter":66,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Asante sana Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia Taarifa iliyoletwa na Sen. Mwaruma ambaye ni Seneta wa Kaunti ya Taita-Taveta. Taarifa hii imekuja wakati mwafaka. Ni karibu miaka mitatu sasa tangu pesa zianze kukusanywa lakini hakuna sheria ya kusaidia serikali za kaunti na jamii zinazoathiriwa na uchimbaji wa madini."}