{"id":966516,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/966516/?format=json","text_counter":15,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":"Jambo la pili ni kwamba, niko na imani kwamba yale ambayo wamekuja kujifundisha hapa ndani ya Seneti – kujua kanuni na jinsi gani kazi inavyoendelea ndani ya Seneti – wakirudi nyumbani, watakuwa wamejifundisha. Wakiwa wamejifundisha na kuelewa, basi wakirudi kwao, pia wataweza kutekeleza wajibu wao ambao walichaguliwa na watu mashinani ili waweze kuwasaidia ndani ya County Assembly . Vile vile, natumai kwamba wale wafanyikazi wataweza kupata nafasi kwenda katika ofisi mbalimbali ndani ya Seneti, na kuweza kujifundisha."}