{"id":966606,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/966606/?format=json","text_counter":105,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":"Jana alikuwa mahabusu. Karibu sana ndugu yangu. Vile vile, nilikuwa nataka kusema ya kwamba, katika hilo swala ambalo limeulizwa kuongezwe; ni lini ile barabara ya kutoka Mombasa hadi Malindi itamalizika. Kwanza ile sio barabara. Ni barabara ambayo inasafirisha watalii wengi, lakini utaona kwamba, ile barabara imeachwa ni kama pwani sio Kenya."}