{"id":976126,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/976126/?format=json","text_counter":170,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Zawadi","speaker_title":"","speaker":{"id":13176,"legal_name":"Christine Zawadi Gona","slug":"christine-zawadi-gona"},"content":"Wajua mahali pengine hapana mjadala. Upende, ukatae; mwanamke ni kiumbe muhimu. Kama ulikuwa wa maana sana, mbona ubavu utolewe nitengezwe mimi, na ulikuwa uko nao mwilini mwako mwenyewe? Kwa hivyo, mwanamke ni kiumbe muhimu; tukubali hilo kwanza. Halafu pia nataka kuishukuru Serikali ya Kenya; pamoja na yote ambayo uko nayo, imenifanya mimi nimekaa hapa Seneti leo. Hii ni kwa sababu ya Serikali ya Kenya na vyama vyetu tulivyo navyo."}