{"id":983850,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/983850/?format=json","text_counter":215,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":"Asante, Bi. Spika wa Muda. Sijui kama hilo ni Jambo la nidhamu ama ni maelezo. Sisi sote ni binadamu na vile vile tunaweza kupatikana na Virusi vya Korona au COVID-19. Hakuna aliye mjasiri mbele ya ugonjwa. Kwa hivyo, ni muhimu pia sisi kuenda mashinani kukutana na wananchi tunaowakilisha katika Seneti, ili waweze kutueleza masaibu wanayoyapata."}