{"id":994124,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/994124/?format=json","text_counter":218,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Siku hizi imekuwa ni mtindo kwamba kila Saa Tisa Serikali inatoa tarakimu za watu walioambukizwa COVID-19 na vile vile waliopona. Tarakimu hizo hazisaidii kuhakikisha kwamba maambukizi yanapungua, isipokuwa yameweza kuongezeka na inakuwa shida kwa wataalamu wetu kutoa mwongozo kamili ni vipi tutaweza kupambana na Virusi vya Korona."}