{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=135606","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=135604","results":[{"id":1372461,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372461/?format=json","text_counter":33,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Proceed, Sen. Onyonka."},{"id":1372462,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372462/?format=json","text_counter":34,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"Asante Bw. Spika wa Muda. Kila wakati Sen. Cherarkey anapozungumza siasa anamkumbuka Mzee Raila Odinga. Sijui kama akiwa kitandani na bibiye pia Mzee Raila huingia pale kati kati kumsumbua na kuharibu hewa yake. Kwa kinaga ubaga, swala la ardhi ni jambo ambalo limeletwa katika Bunge hili la Seneti. Zamani nilifikiri kuwa maswala haya huyasumbua wakaaji wa Pwani, watu wa eneo la Bonde la Ufa au wakaazi wa Kaunti ya Nairobi City. Shida tunayo nchini kwetu ni kuhusu swala hili la ardhi. Lazima kama Bunge la Seneti tujipange na tuhakikishe tunatumia kamati husika na kuhakikisha suluhisho la kudumu limetafutwa ili tumalize shida hizi za ardhi nchini. Bw. Spika wa Muda, ugumu umeingia haswa baada kwa Mheshimiwa Rais William Ruto alipoleta ratiba ya kujengwa kwa nyumba katika maeneo wakilishi ndani ya kaunti zote nchini. Eneo la Trans Nzoia ni mojawapo ya maeneo yaliyo kwenye Bonde la Ufa. Juzi kulikuwa na matangazo kuwa Rais alielekeza waliyo na shamba zilizokuwa za serikali zamani na zilizokuwa zimesimamiwa na Idara ya Jela zirudishwe ili zithibitiwe na Serikali. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."},{"id":1372463,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372463/?format=json","text_counter":35,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"Katika Kaunti ya Kiambu, hususan eneo la Thika, kuna shida inayohusu shamba la Del Monte. Hadi sasa hakuna jawabu. Tukirudi katika Bonde la Ufa, Sen. Cherarkey na wenzetu wamefanya kazi nzuri sana. Wakaazi wa Kaunti ya Kericho pamoja na kampuni za ukuuzaji chai wanazungumzia swala la ardhi. Bw. Spika wa Muda unatoka eneo hili na nimeona ukiyashughulikia mambo haya. Nawasihi waliyo na fursa ya kuongea na Rais pamoja na Mawaziri wanao kushughulika na mambo ya ardhi, watupe ruhusa ya kuangalia maswala ya ardhi na migogoro ambayo imetokea ili kama viongozi, Rais wa nchi yetu na wahusika wote tujaribu kupata suluhisho kwa heshima, haki na kisheria. Hili ndilo jambo ambalo ningetaka kuuliza ndugu zangu ambao wako hapa. Ingewezekana, Seneti ingejaribu kutatua mizozo ya ardhi katika nchi hii. Tuichukue kamati na tujihusishe ili tutafute suluhisho. Ukiona vile Wakenya wanafurushwa kutoka makaazi yao, wanaambiwa court"},{"id":1372464,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372464/?format=json","text_counter":36,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"order"},{"id":1372465,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372465/?format=json","text_counter":37,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"imefurushwa, au askari wamepewa chai na hawawezi kwenda kuhakikisha kuwa ile"},{"id":1372466,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372466/?format=json","text_counter":38,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"court order"},{"id":1372467,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372467/?format=json","text_counter":39,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"ya kuwazuia kubomoa nyumba imetekelezwa. Haya mambo yote yatafanya wananchi na wageni ambao wangependa kuleta hela zao ili wakuze rasilimali ya nchi yetu wadidimie kama hatutapata suluhisho kuhusu mambo haya. Kwa kingereza tunasema the Land question in Kenya must be sorted out for us to continue movingeffectively as a country. Tuwe nchi ambayo ina heshima, inafuata sheria na ambayo inampa mwekezaji nafasi ya kuweka mali yake, ajue kuwa wanaweka pesa mahali ambapo sheria inafuatiliwa na hamna shida ya ardhi. Bw. Spika wa Muda, tunapojadili na kuyaangalia haya maswala, Bw. Spika wa Muda umesafiri na kutazama nchi ya Rwanda. Wakenya ndio walitengeneza mikakati hiyo. Ukiwa kule unaweza pata nambari ya shamba, anaye ishi pale, wakati nyumba ilijengwa na pia pesa gani za kiserikali- taxes - ambazo zimelipwa. Pia unaweza kujua kama mwenyewe anataka kuiuza shamba hilo. Utapata habari yote pale. Nani anayetengeneza habari hiyo yote? Ni Wakenya. Lakini ukisema kuwa kama Wakenya tuketi na tujaribu kupata suluhisho kuhusu maswala haya yote, haiwezekani. Kwa sasa, unapata shamba moja lina hati miliki za ardhi 12. Unapata mama mjane ambaye anafukuzwa katika shamba lake. Unapata Chifu pia hawezi kumsaidia. Hili jambo la kusuluhisha shida za shamba nchini lazima liangaziwe. Kamati husika inafaa kujaribu iwezekanavyo ili tuketi Pamoja. Wengi wetu ni wazee na tunafahamu mambo haya. Tutafute suluhisho ili Wakenya wajue kuwa sheria inalinda mali na rasilimali yao. Asante."},{"id":1372468,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372468/?format=json","text_counter":40,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Sen. (Dr.) Murango, proceed."},{"id":1372469,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372469/?format=json","text_counter":41,"type":"speech","speaker_name":"Sen. (Dr.) Murango","speaker_title":"","speaker":{"id":13585,"legal_name":"Murango James Kamau","slug":"murango-james-kamau"},"content":"Asante Bw. Spika wa Muda. Kwanza nataka kusimama na maombi ya wakaazi wa Muthanthara kuhusu maeneo yanayohusu hati miliki ya ardhi. Nimetoka Kaunti ya Kirinyaga, eneo la Mwea. Mwaka 2020, nilimzika nyanya yangu akiwa na miaka 118. Sikuwa nafaa kufanya hivyo kimila, lakini alifaa kuzikwa na kijana wake wa kiume wa kwanza. Kutoka enzi za ukoloni, wakaaji wa Mwea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."},{"id":1372470,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1372470/?format=json","text_counter":42,"type":"speech","speaker_name":"Sen. (Dr.) Murango","speaker_title":"","speaker":{"id":13585,"legal_name":"Murango James Kamau","slug":"murango-james-kamau"},"content":"hawajapata hati miliki ya mashamba yao na wanalazimishwa kuzika watu wote katika makaburi ambayo yamejaa na hayawezi panuliwa kwa sasa. Miaka ambayo imepita, watu wamezaana; watoto na vijana ni wengi. Wanaomiliki mashamba hawawezi kuyagawa mashamba yale kwa watoto wao kama urithi, kwa sababu hawana hati miliki. South Ngariama na Mwea Irrigation Scheme katika Kaunti ya Kirinyaga kuna shida ya mashamba kukosa hati miliki. Ili jamii iimarike kiuchumi lazima tuhakikishe kwamba wale ambao wanalia wapewe hati miliki wapatiwe, kwani zitawasaidia kiuchumi. Ukiwa na hati miliki unaweza pata mkopo kutoka kwenye benki."}]}