{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=135698","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=135696","results":[{"id":1373381,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373381/?format=json","text_counter":203,"type":"speech","speaker_name":"Kitutu Masaba, ODM","speaker_title":"Hon. Clive Gisairo","speaker":null,"content":"Thank you, Hon. Deputy Speaker."},{"id":1373382,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373382/?format=json","text_counter":204,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Deputy Speaker","speaker_title":"","speaker":null,"content":"The Member for Kilifi North, Hon. Owen Baya"},{"id":1373383,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373383/?format=json","text_counter":205,"type":"speech","speaker_name":"Kilifi North, UDA","speaker_title":"Hon. Owen Baya","speaker":null,"content":" Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Mswada ambao upo katika Sakafu ya Bunge leo ni Mswada muhimu sana unaohusu wazee wa vijiji na wazee wa Nyumba Kumi. Ninamshukuru rafiki yangu, Mhe. Malulu Injendi kwa kuleta Mswada huu. Huu ni Mswada ambao mimi niliuleta katika Bunge la Kumi na Mbili lakini haukufanikiwa. Niliuleta tena katika hili Bunge la Kumi na Tatu lakini nikapata ndugu yangu amenitangulia mbele, nikasema tuungane tusukume Mswada wake. Wazee wa vijiji hapa Kenya wanapata shida sana. Wao huamka mapema asubuhi wakimbie kwa ofisi ya chifu ili wafanye kazi ya Serikali. Wao huamshwa usiku wafanye kazi ya Serikali. Kila mtu hutafuta wazee wa kijiji, hata wanasiasa. Wazee wa kijiji wanaporudi nyumbani jioni, wanarudi mikono mitupu. Watu wao hulala njaa ilhali wao hushinda kazini kwa sababu ile kazi wanafanya hawalipwi. Huu ni wakati mwafaka kama Bunge la Kumi na Tatu kuwanusuru wazee wa vijiji. Ninaamini kwamba Serikali iko na pesa. Pesa hizi zikitafutwa, wazee wa vijiji Kenya nzima watapata pesa kwa kulipwa mshahara kama vile wanavyolipwa Assistant Chief na machifu ili nao wakae vizuri maanake wanafanya kazi kubwa sana. Pale kwangu Kilifi North, kuna mzee amefanya kazi ya mzee wa kijiji kwa karibu miaka kumi. Mzee huyo anaitwa Chembakeke. Ametumikia wananchi kama mtu ambaye yuko kazini. Amewacha kila kitu ili afanyie Serikali kazi lakini watoto wake hawaendi shule kwa sababu hana pesa za kuwalipia karo. Huyu mzee hukosa pesa ya kununulia mkewe dawa anapogonjeka kwa sababu yuko kazini akifanya kazi ya Serikali. Pale Chifu na A ssistant Chief wanakoenda, wao hutaka kwenda na wazee wa vijiji na huwa wanaenda nyumbani bila malipo yoyote. Kwa hivyo, wakati mwafaka umefika wa kuangalia wazee wetu wa vijiji ili walipwe. Kila wakati tunapoenda mikutano kama Wabunge, wazee wa vijiji husema kuwa wametufanyia kazi lakini hawajui wataanza kulipwa lini. Kuna wale polisi wa Kenya Police Reserve (KPR) ambao hulipwa marupurupu. Ile kazi wanayofanya ni kama kazi ya wazee wa vijiji lakini wazee wa vijiji hawalipwi chochote. Tukiendelea kuwaacha wazee wa vijiji bila malipo, tutasambaza umaskini. Serikali yetu inafaa ipunguze umaskini, lakini inasambazaa umaskini kwa sababu inaruhusu watu wafanye kazi bila malipo. Wazee wamejitolea kweli kweli kwa sababu wanapenda community . Wanafanya kazi zao kwa kujitolea lakini mwisho wa siku wanaenda nyumbani bila chochote na familia zao zinabaki kwa umaskini. Serikali haiwasaidii hawa wananchi. Siku moja nilisema kuwa ni afadhali ikiwa hawa wazee wote wataacha hizi kazi. Wanaweza kutafuta mambo mengine ya kufanya ambayo yatawapa mapato. Siku saba za wiki, wazee wa vijiji huwa kazini wakiwahimiza watoto wa wazazi wengine waende shule, haswa wakati huu ambao tunaongea kuhusu 100 per cent transition . Ni wazee wa vijiji ambao huzunguka kila mahali wakiwaambia watoto waende shuleni ilhali watoto wao wanabaki nyumbani kwa kuwa hawana karo na Serikali haiwangalii. At least hata kama hakuna pesa, wazee wa vijiji wajue kuwa wana privilege fulani. Kwa mfano, hata kama watakosa pesa, wajue kuwa watoto wao watasoma bila kuulizwa karo. Watoto wao watasomeshwa kwa sababu wazee wa vijiji wanatumikia Serikali. At least tutasema kuwa hii ni kitu watakacho faidika nacho. Wazee wa vijiji wanapojitokeza kuwatafuta watoto ambao hawajaenda shule ili waende shule, wanapowapeleka watoto hao shuleni, headmasters huwa hawakumbuki kuwa hao ni wazee wa vijiji wawaambie watoto wao wasome shuleni bila kulipa karo. Hao huwaambia walipe karo. Kwa hivyo, hakuna faida yoyote hapa Kenya ya kuwa mzee wa kijiji. Huu Mswada ambao ndugu yangu, Mhe. Malulu Injendi – Mheshimiwa mzuri sana anayewafikiria na kuwajali Wakenya – ameleta, ni Mswada muhimu sana. Ninaomba Bunge hili lipitishe huu Mswada. Bajeti itakapoandaliwa mwaka huu, tuwaambie wanakamati wa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi Pamoja na Mhe. Ndindi Nyoro kuwa ni lazima waweke bajeti ya wazee wa vijiji katika bajeti ya mwaka huu ili wazee wa vijiji wazidi kufanya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"},{"id":1373384,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373384/?format=json","text_counter":206,"type":"speech","speaker_name":"Kilifi North, UDA","speaker_title":"Hon. Owen Baya","speaker":null,"content":"kazi na wapate pesa ya kukimu maisha yao na familia zao. Ninakumbuka nilipopendekeza Mswada huu, kuna mambo yaliyojitokeza. Usipolipa wazee wa vijiji pesa, utakuwa unasambaza corruption kwa sababu, wazee wa vijiji watakapokuwa wanakutana kwa mabaraza ya kuamua kesi, watakuwa wanaambiwa watapewa “kitu kidogo” ili waamue kesi kwa manufaa ya wachache. Kwa sababu hawalipwi, wazee wataanza kutafuta pesa kwa njia zingine ambazo hazifai. Ikiwa tutaendelea kuwa na wazee wa vijiji wanaofanya kazi bila kulipwa, tutakuwa tunaleta ufisadi katika hizo kazi. Kama wazee watafanya kazi na wasilipwe wanapoamua kesi katika mabaraza, atakao wapa “chai” ndiye atakayepata haki. Yule ambaye hatakuwa na chochote hatapata haki. Kwa hivyo, tuwafanyie haki wazee wa vijiji kwa kuwalipa. Tusipowalipa, watatafuta mbinu na njia za kupata pesa ambazo si halali. Tukitaka kumaliza corruption katika wazee wa vijiji, ni lazima walipwe. Ninataka kuwa katika mstari wa mbele kwa kusema kwamba, katika bajeti ambayo tutapitisha, wakati ambapo Budget Policy Statement (BPS) itakapokuja kuwe na line itakayosema kuwa ni wakati mwafaka wa kuwalipa wazee wa vijiji na hali hio iendelezwe mpaka itakapoingia kwa bajeti. Tunaiambia Kamati ya Administration and National Security inayoongozwa na Mhe. Tongoyo ikae kidete. Wakipewa fursa ya kutengeneza bajeti, waweke pesa ya wazee wa vijiji iwe Ksh 5billion, 8 billion au 10 billion per year . Kenya ilitumia Ksh10 billion kufanya maneno ya “reggae.” Ten billion ilitumika kwa Building Bridges Initiative (BBI) . Hiyo Ksh10 billion ipatiwe wazee wa vijiji. Tukiwapa bajeti, tuhakikishe kwamba kuna usalama na utulivu katika hii nchi na vijiji vyetu vinakuwa managed vizuri. Huo ndio mchango wangu katika maneno ya wazee wa vijiji. Kwa hivyo, ninafurahia kuwa tumeleta huu Mswada kwa Second Reading . Tuupitishe kabla bajeti haijamalizwa katika hili Bunge ili wazee wa vijiji waanze kupata matunda ya kazi yao. Ninaunga mkono mia fil mia Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Malulu Injendi, mtu mzuri. Asante."},{"id":1373385,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373385/?format=json","text_counter":207,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Deputy Speaker","speaker_title":"","speaker":null,"content":"The Member for Kitui South, Hon. Rachael Nyamai."},{"id":1373386,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373386/?format=json","text_counter":208,"type":"speech","speaker_name":"Kitui South, JP","speaker_title":"Hon. (Dr) Rachael Nyamai","speaker":{"id":13374,"legal_name":"Richard Ken Chonga Kiti","slug":"richard-ken-chonga-kiti"},"content":" Asante sana, Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia swala hili muhimu ambalo limeletwa na Mhe. Malulu Injendi. Kabla sijachangia, ningependa kuchukua fursa hii kuwatakia wakatoliki wa constituency ya Kitui South, Wakenya na dunia nzima Jumatano ya majivu yenye baraka. Pia, ninawatakia wakati mzuri wa lent. Ninachukua fursa hii kuwashukuru wanawake wa Bunge leo kwa kuvaa nguo nyeusi kwa kuwakumbuka wasichana na wanawake wetu ambao waliuwawa katika hali tatanishi katika nchi yetu ya Kenya na sehemu zingine za dunia. Wazee wa vijiji ni jambo ambalo limezungumziwa sana katika Bunge hili lakini hatujachukua step kubwa ya kuwapa kiinua mgongo chao ama kuwalipa kwa kazi wanayoifanya. Hawa ni wazee na wengine wao ni wazee waliopitisha miaka sabini. Ninashukuru Serikali kwa sababu wengine wao wanapata pesa ya uzeeni kutoka kwa Serikali. Hata hivyo, wazee wa vijiji wanafaa kushughulikiwa wakati huu kwa sababu hao ndio hukutana na mambo mabaya ambayo hufanyika katika vijiji vyetu. Mhe. Naibu wa Spika, wamekuwa wakifanya kazi hii. Wengine wamefanya miaka kumi na kumi na mitano. Wengine wamefanya kazi hii tangu wawe watu wazima. Kwa hivyo, ningependa kushirikiana na wenzangu. Huu ni wakati wa Serikali ya Kenya Kwanza kuwezesha wazee wa vijiji wapatiwe pesa, ili tuwashukuru kwa ile kazi wanafanya kila siku wakiwa na machifu na manaibu wao. Tunajua kwamba machifu na manaibu wao wanapatiwa pesa kila mwezi na mafuta ya kwenda mahali kuna matukio. Hawa wazee wamejitolea kwa miaka mingi. Kwa hivyo, ningependa kushirikiana na Wabunge wale wamezungumza mbele yangu. Tuwapatie pesa ndio waone kazi ambayo wamekuwa wakifanya ni muhimu. Saa hii tunazungumzia kuhusu social health insurance. Wazee hawa watasaidiana na Serikali ili watuambie ni nani anaweza lipa hii mia tatu ambayo italipwa na ni nani hawezi katika jamii. Kwa hivyo, hawa wazee wa vijiji ni muhimu sana The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"},{"id":1373387,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373387/?format=json","text_counter":209,"type":"speech","speaker_name":"Kitui South, JP","speaker_title":"Hon. (Dr) Rachael Nyamai","speaker":{"id":13374,"legal_name":"Richard Ken Chonga Kiti","slug":"richard-ken-chonga-kiti"},"content":"katika kusukuma mbele mambo ya social health insurance. Pia, hawa wazee wanatumiwa sana kueneza mambo ya Serikali zote katika nchi ya Kenya. Katika Serikali hii, wataeleza watu umuhimu wa ujenzi wa nyumba na sera zote. Ninaunga mkono wapatiwe kiinua mgongo na tuwashukuru kwa kazi nzuri ambayo wanafanya. Hata tukizungumzia mambo ya ushauri, hawa wazee ndio wanafika kwanza mahali mtu amekufa ama ameuawa. Wasichana wengi wanauawa katika hoteli wakati huu. Pia, wanafika wakati watu wamepigana na kuumia. Hatufikiri shida wanapitia akilini. Hata kama hakuna kitu kingine tutawafanyia, wacha tuwapatie pesa ndio waone kazi wanafanya ni muhimu nchini. Wengi wamengojea sana. Wale wana miaka themanini wamengojea kwa miaka ishirini. Wale wana miaka sabini, wamengoja tangu wawe na miaka hamsini. Ninaomba Kamati ya Bajeti ambayo inasimamiwa na Mhe. Ndindi Nyoro na Kamati ya Idara ya Utawala na Usalama wa Taifa ambayo inasimamiwa na Mhe. Tongoyo washikane. Pia, sisi sote tuseme wazee wa vijiji ni muhimu sana katika Kenya yetu. Wanaangalia mambo ya nyumba kumi na wasichana ambao wamepata mimba na hawajaenda shule. Pia, wanapeana ripoti ya wazazi ambao wamekataa kupeleka watoto wao shuleni, ili asilimia mia moja ya watoto kutoka shule za msingi wajiunge na shule za upili. Mhe. Naibu wa Spika, ninashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Ninaunga mkono kabisa kwamba wazee wa vijiji watambuliwe kwa maneno na wapatiwe kiinua mgongo. Asante."},{"id":1373388,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373388/?format=json","text_counter":210,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Deputy Speaker","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Member for Migori, Hon. Fatuma Mohammed."},{"id":1373389,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373389/?format=json","text_counter":211,"type":"speech","speaker_name":"Migori County, Independent","speaker_title":"Hon. Fatuma Mohammed","speaker":null,"content":" Mhe. Naibu wa Spika, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili nipeane maoni yangu. Ninawaambia wenzangu wote happy new year. Tunashukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kurudi salama sisi sote na afya nzuri. Hawa wazee wanachangia katika jamii. Wanajua watu wa vijiji kuliko hata polisi na wakuu zaidi ambao wanalipwa. Wao niwamaana sana kwetu. Tukitaka kushika mwizi, wanajua kabisa mwizi ni nani. Saa zingine, mahakama inapata nafasi, lakini inakosea kumtambua yule mbaya. Mzee wa Kijiji anajua familia kuanzia utotoni. Anaweza shuhudia na aseme Fatuma amekuwa mtu fulani tangu azaliwe na ukweli upatikane. Wanachukua fursa nyingi sana. Ni kama watu ambao wanafanyia Mungu kazi kwa sababu hawalipwi chochote. Wanaishi maisha mabaya. Ni maskini hata kuliko wanaowafanyia kazi. Tunahimiza Serikali ya Kenya ichukue nafasi kubwa sana kuwatetea hao wazee, ili wazidi kutusaidia. Wakati mambo ya ugaidi yalizidi sana, wazee walitusaidia sana kutambua vijana wabaya na wazuri. Pia, wanatusaidia kuhimiza utamaduni wetu. Kila siku wanafunza wadogo wetu. Wanatuambia utamaduni wetu ulianzia wapi na unaelekea wapi. Kwa hivyo, hawa wazee wanafaa kuchungwa. Zaidi ya haya, kwa sababu ya umri wao, wana afya ambayo sio nzuri, lakini hawawezi kupata matibabu hata katika hospitali za Serikali. Ninaomba matibabu ya wazee ipewe kipaumbele ili watibiwe hospitali bila malipo yeyote. Hawana bima na Serikali haitaweza kuwalipia. Ikiwezekana, walipiwe bima ama wapewe fursa ya kuingia hospitali yeyote kutibiwa pamoja na familia. Tukiongea kuhusu wazee, tusifikirie ni wa kiume peke yake. Kuna wa kike pia. Watambulike na wapatiwe nafasi ya kupata malipo madogo ya kujimudu kwa kuwa ile kazi wanafanya kwa jamii hawawezi kulipwa mshahara wa kutosha. Ni kuwashukuru tu kwa kazi wanayotusaidia katika jamii. Kama Serikali na Bunge la Kitaifa, tujaribu tupitishe Mswada ambao utawezesha hawa wazee wapate nafasi nzuri ya kutusaidia na motisha ya kufanya hii kazi. Tusipowapatia kitu kidogo cha kujimudu, tunaeneza ufisadi, kwa sababu itabidi waombe watu kuku ndio wafanye ile kazi wanafaa kufanya. Wanapotaka kusafiri, hawana nauli. Inabidi waombe. Hiyo inakaa ni kama mzee anakuomba hongo. Hawa ni wazee ambao wanahekima, heshima na hawataki waonekane ni kama wanaomba. Serikali ijaribu sana tuwatetea hawa wazee. Itakuwa baraka kwetu kama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"},{"id":1373390,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1373390/?format=json","text_counter":212,"type":"speech","speaker_name":"Migori County, Independent","speaker_title":"Hon. Fatuma Mohammed","speaker":null,"content":"watu wadogo ama Bunge la Kitaifa ambalo litapitisha kuwa wazee wamepata nafasi nzuri ya kuweza kujimudu katika jamii yetu. Mungu awabiriki wote."}]}