{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=135995","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=135993","results":[{"id":1376351,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376351/?format=json","text_counter":236,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."},{"id":1376352,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376352/?format=json","text_counter":237,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"walikutana katika Kamati na kuweza kujadili haswa Kiongozi wa Waliowengi, Sen. Cheruiyot, Sen. Omogeni pamoja na wale wengine. Naunga mkono mapendekezo waliotoa kuhusu Constituencies Development Fund"},{"id":1376353,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376353/?format=json","text_counter":238,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"(CDF)"},{"id":1376354,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376354/?format=json","text_counter":239,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"na County Assemblies Fund (CAF ) na Senate Oversight Fund . Vile, naunga mkono ofisi ya Kiongozi wa Upinzani na mapendekezo walioileta katika tume hii ya uchaguzi. Ni kinaya kwa sababu mambo waliojadili yangejadiliwa katika Bunge hili bila kuupoteza muda. Msingi tunaouweka katika nchi hii wa kusema ni lazima kuwe na vurugu, fitima na hali isiyo hali katika nchi yetu ili tupatane kujadili mambo haya inavunja moyo sana. Kwa mfano; mapendekezo haya yote yangeweze kutolewa kwa Kamati husika za Bunge. Waliokuwa wanaongoza Kamati hii ya majadiliano ni watu walio Bunge hili. Waliosema kuwa maoni hayo yote yangejadiliwa katika Bunge hili waligonga ndipo. Tukiuweka msingi kama huu eti kila wakati ni mvutano kama ule wa 1997, Inter-PartiesParliamentary Group (IPPG) reforms, kulikuwa na mvutano na ndio maana watu waliketi chini kuzungmza. Ijapokuwa nawapongeza viongozi wale kwa kupata nafasi ya kuketi chini, tumekuwa tunaketi hapa na Kiongozi wa Waliowengi, Sen. Cheruiyot, pamoja na Seneta wa Kaunti ya Nyamira, Sen. Omogeni. Wangeketi na kuongea kuhusu jambo hili. Mambo haya yakiwekwa katika kumbukumbu itaonekana kuwa tulikuwa hatuelewei mambo tuliyopaswa kufanya. Mapendekezo ambayo wameleta hapa kwenye ripoti, tungeyazindua katika Bunge hili na kuibadilisha Katiba. Naunga mkono nikijua kuwa hakuna siku hata moja hatujaongea na Sen. Oketch Gicheru, aliye upande wa upinzani na mimi upande wa Serikali. Tulikuwa tukiiongea kwa utulivu tulipopatana kwenye Kamati tunapokutana. Maneno ambayo yanasemwa kuwa viongozi wanapatana kwa sababu ya kuleta utulivu basi ni kinaya kwa sababu Sen. Cheruiyot anaongea na Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Mheshimiwa Opiyo Wandayi. Ni vizuri tuzichunge rasilimali zetu. Baadala ya sisi tuliochaguliwa kuchukua fursa na majukumu tuliyopewa na kufanya tunayopaswa, wengi wanasema kuwa walienda kujadiliana kuhusu gharama ya maisha. Utaongea aje kuhusu gharama ya maisha ilhali hayo mambo yalikuwa yamezingatiwa vizuri na Serikali. Serikaili ilikuwa imeweka misingi dhabiti. Tayari mbolea ilikuwa imepunguzwa bei pia. Gunia za mahindi ambazo zimevunwa kwa sababu ya mbolea iliyotolewa ni nyingi. Tunaweza kusema na kufanya mengi ili kupongeza Kamati hii. Lakini, nikiyaangalia mapendekezo hayo katika riporti hii ya kurasa 500, nina uhakika tungefanya mambo haya yote katika Bunge hili. Tunawakosea Wakenya heshima na shukrani kwa sababu walituchagua kufanya kazi hii. Badala ya ndugu zetu, Sen. Cheruiyot na Sen. Omogeni kuifanya kazi hii hapa, moja kwa moja, kiguu na njia wanaenda kuifanyia Bomas of Kenya . Ni swala linalovunja moyo na sio kwangu tu lakini kwa Wakenya wote. Nawapongeza kwa kufanya kazi nzuri. Lakini, wangeifanyia katika Bunge ili wachunga mali ya Wakenya. Swala ambalo lingekuwa bora zaidi. Kusonga mbele, msingi tunaoweka si mzuri na unavunja moyo wangu kwa Wakenya wote."},{"id":1376355,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376355/?format=json","text_counter":240,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."},{"id":1376356,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376356/?format=json","text_counter":241,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Wakenya waliouwawa katika maandamano walisaidika vipi na mapendekezo haya tunayoleta hapa? Tutawaambia nini? Mali yao itaregeshwa vipi? Ni vizuri tunene ukweli na sio kuficha ukweli kwa kusema mengi. Walakini ilileta utulivu. Mswahili alisema wengi wape. Naunga mkono Ripoti hii. Lakini, isiwe naimsingi ambao utakuwa wa madhara kwetu."},{"id":1376357,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376357/?format=json","text_counter":242,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mumma","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Proceed, Sen. Faki"},{"id":1376358,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376358/?format=json","text_counter":243,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Asante, Bi Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono ripoti ya Kamati ya uwiano ambayo iliwasilishwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge hili. Kwanza, natoa pongezi kwa viongozi wawili wakuu ambao walikubaliana kuwe na Kamati hii. Vile vile, wanakamati wote waliofanya kazi pamoja na watumishi wao kuhakikisha kuwa wameitoa ripoti inayokubalika. Najiunga na katibu wa chama chetu cha Orange Democratic Movement (ODM). Hata kama Ripoti hii ina mambo mengi ambayo yamezungumziwa, kuna mambo msingi ambayo hayakutajwa na kuzungumziwa kwa ufasaha. Moja wapo ikiwa ni kuongezeka kwa bei ya bidhaa muhimu katika nchi yetu. Yani gharama ya maisha imeongezeka maradufu kiasi ambacho wengi katika nchi ya Kenya hawawezi kuandaa mkate wala ugali katika meza zao kila siku. Hilo ni jambo muhimu sana. Kuongezeka kwa gharama ya miasha kuna sababisha watu kukosa namna ya kujikimu kimaisha. Wanafunzi wanakosa kwenda shule na wagonjwa wanakosa matibabu na hayo yote yanasababishwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa muhimu na maisha kwa jumla. Kwa mfano, kuongezeka kwa gharama ya Value Added Tax (VAT) ya mafuta. Swala hili lilikua hapo awali, 2018 na 2019. Serikali iliyokuwa wakati ule ili leta mswada katika Bunge la Kitaifa na ika punguzwa kutoka asilimia 16 hadi Asilimia 8. Hivyo ilisababisha kupunguka pakubwa kwa bei za bidhaa muhimu kama mafuta na zinginezo. Bi. Spika wa Muda, tukiangalia katika magazeti yetu kila siku kuna ripoti kadha wa kadha ambazo zinaonyesha ubadhirifu wa pesa za umma katika nchi yetu. Leo utasikia kuna millioni 600 za kurekebisha nyumba ya Naibu wa Rais. Hizi ni pesa za umma ambazo zinavujwa na kutumika kwa hali ambayo isiyo ya kisawasawa. Upande mwingine, wale walala hoi wanaendelea kupata shida ya kusomesha watoto wao. Watoto wengi wanakosa kusoma na baadaye wanakuwa majambazi na hali yao ya maisha inabadilika. Wenzetu wa upande ule mwingine wamesema kuwa kulikuwa na vurugu kabla ya Kamati hii na wale ambao mali yao iliharibiwa walipwe fidia. Watu wengi walipoteza maisha yao. Wengine walipigwa risasi na kuuliwa na vikosi vya usalama. Kiongozi wa Walio Wachache alishikwa akitoka hapa Bunge akienda nyumbani kwake. Kushikwa kwake kuliwapa furaha wanadada wengi. Baadhi ya Maseneta katika Bunge hili waliona raha walipomuona Sen. Madzayo ametiwa mbaroni na hali ambayo ilionyesha ni mtu wa kisawasawa."},{"id":1376359,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376359/?format=json","text_counter":244,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."},{"id":1376360,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1376360/?format=json","text_counter":245,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Mojawapo wa vipengee muhimu vya hii ripoti ni suala la Bunge kuangalia gharama ya maisha. Kwenye mchakato wa kutengeneza bajeti ya mwaka 2024/2025, gharama ya maisha lazima ipunguzwe. Suala la pili ambalo ningependa kuliguzia ni kuongezeka kwa akina mama kwenye uongozi wa nchi. Hili ni suala ambalo limekuwa donda sugu. Bunge lililopita, lilijaribu mara tatu kupitisha Mswada huu lakini haukupita. Nakubaliana na Kamati kwamba lazima watu wakae chini kama Bunge kuhakikisha kwamba suala hili linatekelezwa ili watoto wetu wa kike; dada zetu wapate fursa ya kuingia katika uongozi. Tunapoelekea itakuwa ni ngumu zaidi kwa kina dada kuingia katika uongozi wa kuchaguliwa. Kila siku wale ambao wanahusika kama viongozi wa vyama ama wale ambao wanasimamia vikundi hivi wanatumia mbinu ambazo hazifai kikatiba kuzuia wasichana kupata uongozi. Jambo la mwisho ambalo ningependa kuligusia ni kuhusu hazina ambazo ziko. Kwa mfano, hazina ya National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF), ambayo imesaidia pakubwa kupeleka maendeleo mashinani. Tumekubali hapa kwamba hazina ya Seneti ya oversight imefanya kazi kubwa muda mchache tangu ipitishwe. Tungependa Ward Fund (WF) iwepo ili kila wardi iweze kupata maendeleo kutoka kwa serikali za kaunti zetu. Baadhi ya wadi hazipati maendeleo kwa sababu magavana hawaelewani na wabunge wa Bunge za kaunti. Kila wadi iwe na pesa zake kuhakikisha kwamba maendeleo yanafika pembe zote za wadi zetu. Tunakubaliana kwamba ipo haja kuangalia kwa haraka masuala ya mipaka ya maeneo Bunge na vilevile wadi. Hili ni swala la kikatiba na lingekuwa limeshughulikiwa kabla ya mwaka 2022, lakini halikufanyika kwa sababu za kiserikali na kifedha. Ni lazima hili jambo lifanyike ili maeneo ambayo yanastahili kupata maeneo zaidi ya ubunge yaweze kuyapata ili wananchi waweze kupata uwakilishi wa uhakika katika mabunge ya kaunti na vilevile Bunge la Kitaifa. Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii."}]}