{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=136226","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=136224","results":[{"id":1378661,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378661/?format=json","text_counter":317,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Equalization Fund"},{"id":1378662,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378662/?format=json","text_counter":318,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":". Lakini mwanakandarasi alienda kujenga pahali padogo kisha akakimbia. Sasa huwa ni hasara kwa Serikali kwa sababu ya pesa ambayo imetumika. Maji bado inaingia mbele na kuvunja mpaka ambapo pesa ilitumika. Hiyo ni hasara kwa Serikali na wananchi wetu bado wanapata shida. Jambo hilo linasikitisha. Maji ikiingia, inaenda hadi kwa jiko, inabeba sufuria na inaenda nazo baharini kwa sababu mtu alipewa pesa na hakumaliza kazi. Kisha unashangaa mpaka sasa hujamwona mwanakandarasi huyo, hayuko kortini wala haujui mahali alipo. Hata ukiulizia kwa Wizara, hiyo projec t, unaambiwa haijulikani na kitu kilijengwa na dhibitisho liko kwa sababu kuna kipande nusu. Lakini itakuwa vizuri kwa Ripoti hii kuhakikisha kwamba yule ambaye alipokea pesa au kama Serikali itajenga tena, ihakikishe imejenga kwa njia ambayo itadhibiti kile kipande kidogo kilichopo ili kisiharibike. Mhe. Spika wa Muda, kijiji kingine ni Kizingitini. Huko kuna ngome lakini ngome ni nusu. Shule zinabebwa na maji kwa sababu ya mwanakandarasi au pesa iliyotolewa haikuwa kamili. Kwa hivyo, hii Ripoti ikipelekwa kwa Kamati ya Utekelezaji, ihakikishe imefuata hii miradi ambayo haikukamilishwa ili miradi yote iweze kukamilishwa."},{"id":1378663,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378663/?format=json","text_counter":319,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":"Mhe. Spika wa Muda, kuna kijiji kama Faza, pia kimejengwa vya kusikitisha. Kwa nini mradi usijengwe kikamilifu ili watu wapate kusaidika? Utaona kila kijiji miradi ni nusu, na haijakamilika na wananchi wanasumbuka. Ile nusu iliojengwa haisaidii. Ikikamilishwa ndio itasaidia. Itakuwa ni muhimu hata hii Kamati ya Utekelezaji izunguke Kenya na iangalie hiyo miradi ambayo Ripoti inaangazia kuwa haijakamilika."},{"id":1378664,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378664/?format=json","text_counter":320,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":"Miradi ingine inafanywa kwa hadhi ambayo si sawa na jinsi ilivyo kwenye vitabu. Utasikitika kuwa pesa ya Serikali inajenga mradi na kwa miezi mitatu, huo mradi umeharibika. Kwa mfano, kwetu kuna mradi wa ngome ambao ulifanywa Mkokoni. Watu wanashangaa nazungumzia ngome sana na hawaelewi. Ngome ni seawall ambayo inazuia bahari isiende ikasomba kijiji ikaenda nayo. Kuna ngome ambayo imejengwa, na baada ya miezi mitatu, imeanguka. Inaonyesha pesa hapo zimefujwa. Kwa hivyo, hii Ripoti pia iangazie mambo kama hayo na Mwenyekiti yuko hapa afuatilie."},{"id":1378665,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378665/?format=json","text_counter":321,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":"Mhe. Spika wa Muda, kuna tatizo lingine kwa walio kwenye mamlaka. Kama ni vinara wa kamati au wale wa ofisi za Serikali, miradi inaenda kwa walio wengi. Hilo ni tatizo kubwa. Sisi wa Lamu Mashariki, hata huu mgao wa National Government Constituencies Fund (NG- CDF), watu wakisikia hapa, Lamu Mashariki ndio inapata kidogo zaidi. Lakini utaona kuwa mtu ambaye yuko kwenye kamati, au kwenye nyadhifa za katibu ama waziri, pesa zinapelekwa sehemu zao. Ikipelekwa sehemu zao, sisi kule tunazidi kukaa nyuma."},{"id":1378666,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378666/?format=json","text_counter":322,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":"Kwa mfano, ni kama upande wa utalii. Pesa zinapelekwa sehemu nyingine hadi unashangaa. Ukiangalia katika Bajeti, pesa zinaenda kwa utalii katika sehemu hakuna utalii. Ukiangalia Lamu, kuna mambo mengi yanayoweza kuvutia utalii wetu na watalii waje wengi. Lakini kwa kuwa hakuna waziri huko, basi pesa haiendi kule ili kuvuta watalii waje wengi. Sisi Lamu, tuna sehemu nyingi ambazo zinaweza kuvutia utalii. Kuna sehemu unaweza kwenda na usahau kurudi kwenu na nyingine unaweza angalia dolphins . Kuna sehemu Lamu pekee unaweza ukaenda asubuhi kwa bahari huko deep sea fishing na mchana au jioni ukaenda The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"},{"id":1378667,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378667/?format=json","text_counter":323,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":"kuangalia wanyama wanaogelea, na ni kweli kuna wanyama kama simba wanaogelea. Kwa vile ni lazima wavuke zile creeks. Kwa vile hatuna watu wetu kule, utalii kwetu hauinuki. Hii ni kwa sababu watu walioko pale wanafikiria kwao tu na sio kama Wakenya."},{"id":1378668,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378668/?format=json","text_counter":324,"type":"speech","speaker_name":"Lamu East","speaker_title":"Hon. Ruweida Mohamed","speaker":null,"content":"Ukiangalia NG-CDF, ilikuwa mwanzo ikigawanywa sawa kwa sababu maeneo mengine yalikuwa yameachwa nyuma. Mwajua, kwa historia, maeneo yalikuwa yamewachwa nyuma. Ili kuyaleta yale maeneo kuwa sawa na mengine, ilikuwa imewekwa iwe sawa ili kule nako kuinuke kuwe kama maeneo Bunge mengine. Lakini utaona watu wanatukanyaga kwa kuwa hatuko wengi. Mimi ni Mbajuni pekee yangu hapa. Lakini mimi ni Mkenya. Yafaa Wakenya wengine hapa watufikirie maana hili Bunge ndilo linatengeneza bajeti na kuangalia vitabu vya akaunti. Ikiangalia, yafaa kurekebisha lakini kwa kuwa nambari zetu ni chache, lazima tuje hapa kushukuru kwa kile tunachopata kwa NG-CDF. Haki ya Mungu, hamtufanyii haki. Hii ni kwa sababu pesa za Wakenya zinatumika zaidi katika upande wa usalama. Mnatukataza kutekeleza miradi kwetu Lamu lakini pesa hizo zinakuja Lamu katika upande wa usalama. Ukosefu wa usalama haumdhuru mkaazi wa Lamu pekee yake. Magaidi wakipita Lamu wanaweza kufika Nairobi. Mngeamua kuwa kwa sababu tunapata NG-CDF kidogo, basi tusukumiwe miradi mingine. Lakini huwezi kuona mradi mkubwa kwenye Ripoti isipokuwa ile ya Lamu Port-South Sudan-Ethiopia Transport (LAPSSET) Corridor Project . Mradi wa LAPSSET ni wa Kenya nzima, si wetu pekee. Msihesabu pesa zilizotengewa LAPSSET. Watu wetu wanatatizika kule Lamu Mashariki, kwa sababu hakuna barabara wala ngome, lakini LAPSSET inahesabika kama ni ya Lamu. Mpaka sasa, haijamsaidia mkaazi yeyote wa Lamu. Kwa hivyo, kuna haja ya sisi kusukumiwa miradi mingine kama ujenzi wa barabara, ngome, maji na umeme. Mpaka sasa, hatujaunganishwa na Wakenya wengine. Tuko kivyetu. Kile kinachowaunganisha Wakenya ni barabara. Alhamdulillah tunashukuru kuwa Serikali hii imezindua barabara. Kile kinachowaunganisha Wakenya ni ile national grid . Mpaka sasa, tunatumia majenereta kule kwetu. Sijui kama Kamati hii imezingatia kuwa yale mafuta yanayotumika katika majenereta kule Lamu Mashariki yanafanya bei ya umeme iwe ghali. Laiti mngekubali kutenga Ksh300 milioni ili Lamu Mashiriki iunganishwe kwenye national grid …"},{"id":1378669,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378669/?format=json","text_counter":325,"type":"speech","speaker_name":"Nominated, ODM","speaker_title":"Hon. John Mbadi","speaker":{"id":110,"legal_name":"John Mbadi Ng'ong'o","slug":"john-mbadi"},"content":" On a point of order, Hon. Temporary Speaker."},{"id":1378670,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1378670/?format=json","text_counter":326,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Peter Kaluma","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":{"id":1565,"legal_name":"George Peter Opondo Kaluma","slug":"george-peter-opondo-kaluma"},"content":" What is out of order, Hon. John Mbadi?"}]}