{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=138624","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=138622","results":[{"id":1402641,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402641/?format=json","text_counter":140,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Asante Bwana Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili nitoe kauli yangu kuhusiana na Mswada ambao umeletwa Bungeni na Seneta Cherarkey. Kwanza nampongeza Seneta wa Nandi kwa kazi nzuri anayofanya katika Bunge hili. Tulipompokea hapa mwaka wa 2017, tulimpa wadhfa wa Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Haki za Kibiinadam. Ni hapo tulipoweza kumnoa."},{"id":1402642,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402642/?format=json","text_counter":141,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"(Applause)"},{"id":1402643,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402643/?format=json","text_counter":142,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Kwenye kamati hiyo, kulikuwa na Wakili Fatuma Dullo, Wakili Amos Wako, Wakili Okong’o Omogeni, Wakili Orengo, mimi na wengine. Tulimpa mikoba ambayo anaendelea kuitumia hadi sasa. Kwa hivyo, hawezi kukosea. Vile vile, ningependa nimpongeze kwa kauli aliyotoa jana kuhusiana na jumba la Bunge Tower. Bw. Spika wa Muda, kuna wabunge zaidi ya 400. Wengine watachukuwa ofisi pale kwa kuwa usalama wao ni muhimu sana. Tukija katika Mswada huu, naunga mkono kuwekwa kwa threshold ya thuluthi mbili iwapo unataka kumuondoa mamlakani waziri katika kaunti zetu. Tumeona kwamba mawaziri katika kaunti zetu hawajakuwa na msisimko wa kisawasawa kwa sababu mara nyingi, wanaangalia gavana anafanya nini. Wanapokuwa karibu sana na gavana, Wabunge wa Bunge la Gatuzi wanachukulia kuwa ni unyonge kisha kuwatoa mamlakani kiholela. Hii sheria itasaidia pakubwa kuweza kuleta haki katika wale wanaotaka kuondolewa katika mamlaka ya uwaziri katika kaunti zetu. Bw. Spika wa Muda, tumeona kwamba mara nyingi magavana wanakaba sana kutoa mamlaka kamili kwa waziri. Utapata kwamba waziri mara nyingi anaangalia gavana anasema nini ndiposa afanye kazi. Wanapochaguliwa wanaapishwa kwamba watafanya kazi kulingana na sheria na katiba ya Kenya."},{"id":1402644,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402644/?format=json","text_counter":143,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"(Sen. Beth Syengo walked into the Chamber)"},{"id":1402645,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402645/?format=json","text_counter":144,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Karibu mama orange, naona umeingia. Unahanyahanya mbele yangu wakati nazungumza. Karibu Mheshimiwa. Hii sio lugha mbaya, ni lugha safi ya Kiswahili."},{"id":1402646,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402646/?format=json","text_counter":145,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"(Laughter)"},{"id":1402647,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402647/?format=json","text_counter":146,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1402648,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402648/?format=json","text_counter":147,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Bw. Spika wa Muda, tunasema kwamba ni swala muhimu kuwe na mamlaka ya kuhakikisha kwamba wale wanaoondolewa mamlakani wanatendewa haki. Kumuondoa mtu mamlakani kama alivyoondolewa naibu gavana wa Kisii mwezi uliokwisha ni jambo nzito sana kisheria kwa sababu unamfunga yule mtu kutofanya mambo ya kisiasa na pia kupata kazi serikalini inakuwa ni shida. Kwa hivyo, lazima kuwe na kiwango fulani ambacho kikifikiwa mtu yule anaweza kutoka kwenye mamlaka. Mengi yamezungumzwa kuhusiana na maswala ya kuondoa mamlakani viongozi. Sisi kama Bunge la Seneti tuna mamlaka ya kumuondoa hata Rais. Ila cha kusikitisha, hatuna mamlaka ya kumuondoa waziri katika serikali kuu. Tuliona hapa kwamba kuna mawaziri ambao wana utepetevu mwingi katika kuendesha kazi zao, ila hatuna mamlaka ya kuwaondoa. Naibu wa Kiranja wa Upinzani, Seneta Sifuna, alileta Hoja ya kumcensure Naibu wa Rais lakini haikuona mwangaza. Sina neno la Kiswahili ambalo naweza kutumia kwa sasa ndio maana nikatumia censure ."},{"id":1402649,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402649/?format=json","text_counter":148,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"(An Hon. Member spoke off record)"},{"id":1402650,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1402650/?format=json","text_counter":149,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Kashfa ni kucriticise. Hoja ile haikuweza kuona jua kwa sababu ya yale mamlaka yamewekwa katika Bunge ambayo mara nyingi yanahujumu kazi za Wabunge. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu. Tutasaidiana kuhakikisha kwamba umepita ili tuweke sheria itakayosaidia kuongeza uwazi katika kaunti zetu. Asante Bw. Spika wa Muda."}]}