{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=139579","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=139577","results":[{"id":1412191,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412191/?format=json","text_counter":175,"type":"speech","speaker_name":"Matuga, ANC","speaker_title":"Hon. Kassim Tandaza","speaker":null,"content":"baada ya kupitishwa kwa Katiba 2010. Licha ya kuwa Katiba ilileta mambo mengi mazuri, pia ilileta changamoto. Ilisisitiza sana kwamba kaunti zetu zitengeneze fedha za ndani kwa ndani licha ya ule mgao ambao unatoka kwa Serikali kuu. Hii ilifanya kaunti nyingi kufikiria njia za kuokota pesa kutoka kwa wananchi. Moja ya njia hizo ni kutoa leseni kwa utafutaji wa rasilimali ambazo zinatoka sehemu mbalimbali."},{"id":1412192,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412192/?format=json","text_counter":176,"type":"speech","speaker_name":"Matuga, ANC","speaker_title":"Hon. Kassim Tandaza","speaker":null,"content":"Kama ilivyopendekezwa katika huu Mswada ambao ninaunga mkono, ni jambo la kuhuzunisha kwamba biashara inakuwa ngumu kufanya. Wakati mwingine hata sio biashara tu, hata usafiri. Lori ambalo hata halijabeba kitu likipita kaunti moja hadi nyingine imekuwa ni kama kupitia nchi moja mpaka nyingine. Kwamba, lazima liwe na vibali vya kaunti ambako linaenda licha ya kutozwa ushuru wa ule mzigo ambao limebeba. Hivi vibali ambavyo kaunti zinatoa kwa magari ya mizigo si halali. Tunajua kuwa katika nchi hii, tunayo Wizara inayohusika na kutoa vibali nayo ni Wizara ya Uchukuzi. Na kama ni insurance basi inakua ni ya Kenya nzima. Lakini kaunti zingine zimeweza kutoa vibali vya kadi na kubandika katika magari, kuonyesha gari hili linaruhusiwa kufanya biashara katika eneo lao. Jambo hili halina msingi, bali ni hali ya kuhangaisha wanabiashara. Ni hali ya kufanya bidhaa ziwe ghali zaidi ilhali tunazungumzia ni vipi wananchi wa kawaida wanaweza kupata afueni kibiashara. Nchi hii ni moja na kaunti zililetwa kwa sababu ya kupeleka huduma mashinani. Lakini saa hizi zimekuwa zikiwafinya watu kupitia hizi sheria zao. Kutoka maeneo ya Kwale kuingia Mombasa ni kama ambaye unavuka mpaka wa Lunga Lunga kutoka Kenya kwenda Tanzania. Kwa hivyo, Mswada huu ni muhimu na unahitaji kuungwa mkono na kupitishwa haraka inavyowezekana ili biashara zifanywe bila matata ama pingamizi yoyote."},{"id":1412193,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412193/?format=json","text_counter":177,"type":"speech","speaker_name":"Matuga, ANC","speaker_title":"Hon. Kassim Tandaza","speaker":null,"content":"Mhe. Naibu Spika, jambo jingine ambalo ni la kuhuzunisha ni ufadhili. Kwa mfano, pale Kaunti ya Kwale labda ufadhili utapitia Bandari ya Mombasa ambayo ni kaunti nyingine. Kwa mfano, mtu amenuia kusaidia shule za Kwale kwa kuzipa kompyuta ama vitu ambavyo vitatumika katika darasa. Kisha gari linapofika mpakani kati ya Kaunti ya Mombasa na Kwale pale Likoni yule mfadhili analazimika kulipa ushuru tena licha ya kuwa pengine ashalipa kwa Serikali kuu bandarini. Kaunti bado inahitaji ushuru tena ulipwe ili vyombo viweze kuingia ilhali bidhaa si za biashara - ni mtu binafsi amejitolea kutoa ufadhili kusaidia watu wetu. Lakini yule afisa ambaye amewekwa pale kwenye kituo cha cess anashauri kwamba ni lazima gari lolote linalopita hata ingawa ni la ufadhili lilipe ushuru la sivyo atalifungia. Inabidi mwenye gari azungumze na mstahiki gavana ama mkubwa ambaye anahusika, ili gari liachiliwe. Sisi kama Bunge tuna jukumu la kuona kwamba hali tata kama hizi haziwezi kuendelea. Ikiwa watatoza ushuru basi mtu akiwa ametoka Kilifi akienda Kwale, akilipa ushuru Kaunti ya Kilifi, aweze kubeba risiti kuonyesha tayari ashalipia katika gatuzi moja na anastahili kuubeba mzigo mahali popote pale Kenya. Hii ni kwa sababu nchi ni moja. Alikotoa bidhaa yule mfanya biashara amelipishwa, pengine, Ksh200 na akifika Mombasa analipishwa Ksh800. Akivuka Kwale analipishwa labda Ksh1,000. Je, atapataje faida yake?"},{"id":1412194,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412194/?format=json","text_counter":178,"type":"speech","speaker_name":"Matuga, ANC","speaker_title":"Hon. Kassim Tandaza","speaker":null,"content":"Mhe. Naibu Spika, ninaunga Mswada huu mkono ili uweze kupitishwa mara moja. Magavana wetu licha ya kuwa wana majukumu ya kutafuta hela, wasitafute kwa kuumiza wananchi. Wasifanye maisha yao yawe magumu mpaka wanashindwa kufanya biashara."},{"id":1412195,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412195/?format=json","text_counter":179,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Deputy Speaker","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Member for Kwanza, Hon. Ferdinand Wanyonyi."},{"id":1412196,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412196/?format=json","text_counter":180,"type":"speech","speaker_name":"Kwanza, FORD-K","speaker_title":"Hon. Ferdinand Wanyonyi","speaker":null,"content":" Order! Thank you very much, Hon. Deputy Speaker, for giving me an opportunity to contribute to this very important Bill by the Senate. It is common sense when it comes to finding out…"},{"id":1412197,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412197/?format=json","text_counter":181,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"(Loud consultations)"},{"id":1412198,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412198/?format=json","text_counter":182,"type":"speech","speaker_name":"Kwanza, FORD-K","speaker_title":"Hon. Ferdinand Wanyonyi","speaker":null,"content":"Hon. Deputy Speaker, can you protect me from the crowd that is in front of me? Order! Get out of my way! I am being engaged while I am on the Floor of the House by a passer-by. Can you call them to order? The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor"},{"id":1412199,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412199/?format=json","text_counter":183,"type":"speech","speaker_name":"Kitui South, JP","speaker_title":"Hon. (Dr) Rachael Nyamai","speaker":{"id":13374,"legal_name":"Richard Ken Chonga Kiti","slug":"richard-ken-chonga-kiti"},"content":" On a point of order, Hon. Deputy Speaker."},{"id":1412200,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1412200/?format=json","text_counter":184,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Deputy Speaker","speaker_title":"","speaker":null,"content":"What is your point of order, Hon. (Dr) Nyamai? Let me allow her point of order."}]}