{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=140285","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=140283","results":[{"id":1419251,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419251/?format=json","text_counter":303,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Oketch Gicheru","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Sasa Bw. Spika wa Muda, alijaribu kunikosoa na nikasema ya kwamba ningependa kumsaidia kwa sabubu haelewi mambo ya mpira. Nimesema ya kwamba kabla mchezaji Ouma Chege astaafu alifungia timu yake ya Harambee Stars ambayo ni timu ya Taifa, mabao mengi. Hatuwezi ongea kuhusu Olunga kwa sababu hajastaafu kucheza mpira. Bado anacheza mpira. Ouma Chege alistaafu akiwa amefungia Harambee Stars mabao 35. Oliech alifungia Harambee Stars mabao 34. Ndiposa nilikuwa nasema kabla ya kustaafu. Na unajua kwa sababu yeye ni daktari ambaye hakustaafu kabla kuingia kwa siasa, hajui maana ya kustaafu. Sasa nitamwambia maana ya kustaafu nje ya Bunge. Namalizia kwa kusema, ingekuwa vizuri kwa sababu Katiba, katika Kipengele cha 203 inapatia Serikali ya Kitaifa mamlaka ya kupatia kaunti pesa za ziada wakati wowote ingetaka kufanya hivyo."},{"id":1419252,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419252/?format=json","text_counter":304,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Oketch Gicheru","speaker_title":"","speaker":null,"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1419253,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419253/?format=json","text_counter":305,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Oketch Gicheru","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Mwezi huu tunatengeneza bajeti. Ningeomba kwa niaba ya watu wa Pwani na ndugu yangu Sen. Faki, Serikali iende kwa haraka iwape hii pesa ili waanze kutengeneza hivi viwanja mwezi wa saba au wa nane. Wakati Jumuiya ya Wabunge ya Africa Mashariki watakuja Mwezi wa 12, ingekuwa bora zaidi tuwe na ule uwanja pale Mombasa ili watu wajumuike. Hata wewe Bw. Spika wa Muda Wakili Sigei, juma lililopita nilikuwa kwako. Nilipata umeandaa mchezo mkubwa pale. Uliona vile uwanja ulikuwa umefurika pale Bomet. Vijana, wamama, wazee na jamii yote walikuwa wamekuja kucheza mpira pale Bomet. Hata mimi, nilikuwa niko na furaha zaidi kwa sababu jamii yote ilikuwa imejumuishwa katika mchezo. Ni vyema watu wa Pwani wangekuwa na ile cheche na mbwembwe, haha na hoihoi wakati watakapo pata uwanja mzuri ulio na vifaa vya kisasa wacheze mpira na wajumuike na Wakenya kufurahia kuwa na uwanja mzuri. Kwa hivyo, naiunga hii Hoja ya ndugu yangu Sen. Faki. Ningependa kusema kama kijana barubaru ambaye yuko katika Seneti---"},{"id":1419254,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419254/?format=json","text_counter":306,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Muda wako wa kuendelea umeisha."},{"id":1419255,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419255/?format=json","text_counter":307,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mandago","speaker_title":"","speaker":{"id":13577,"legal_name":"Kiplagat Jackson Mandago","slug":"kiplagat-jackson-mandago"},"content":"Asante Bw. Spika wa Muda. Nachukua nafasi hii pia kuchangia Hoja ya Uwanja wa Manispaa ya Mombasa. Kwanza kabisa niseme mambo ya viwanja katika Taifa la Kenya ni ya muhimu sana. Nikichangia katika Hoja hii ya Sen. Faki ni kwamba, sio Uwanja wa Manispaa ya Mombasa pekee ambao umecheleweshwa. Katika Kaunti ya Uasin Gishu, tuko na uwanja wa kihistoria wa Kipchoge. Sehemu hiyo ndio imetoa wanariadha wengi waliobobea kwa michezo ya kimataifa na kuleta fahari nchi hii ya Kenya. Kwa hivyo, wakati tunakadiria jinsi Uwanja wa Manispaa wa Mombasa utashughulikiwa, pia viwanja vingine kama Uwanja wa Kipchoge Keino kule Eldoret, Kamarin kule Elgeiyo Marakwet County na pia Uwanja wa Kipchoge Keino kule Kapsabet, ni baadhi ya viwanja ambavyo vinafaa kuwa vimeshughulikiwa na Serikali. Pia isitoshe kuwa Serikali ya Kaunti ya Mombasa itumie pesa iliyopewa kwa ugatuzi wa Mombasa kujaribu kuboresha huo uwanja. Mambo ya michezo ni ya muhimu sana kwa viwango vyote hasa vijana. Tukiweza kupata nafasi mahali pazuri pa kufanya michezo, vijana wetu watahepukana na mambo ya mihadarati na upotovu wa nidhamu katika muda ambao wangetumia kufanya michezo uwanjani. Ninaunga mkono Hoja hii na kusema kuwa wanapongojea fedha kutoka kwa Serikali Kuu hata wao kama Serikali ya Ugatuzi ya Mombasa waweze kuiweka kwa orodha ya kwanza kwa baadhi ya mambo ya maendeleo ambayo wanafaa kuyatekeleza kwenye kaunti yao. Naunga mkono."},{"id":1419256,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419256/?format=json","text_counter":308,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Hon. Senators, that brings us to a close on the contributions to this particular Motion, and there being no other person interested in contributing, I will call upon Sen. Faki, to reply."},{"id":1419257,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419257/?format=json","text_counter":309,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1419258,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419258/?format=json","text_counter":310,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kujibu hoja zilizotolewa na Maseneta kuhusiana na Hoja hii ya Kuidhinishwa kwa Ruzuku ya Masharti kwa Ujenzi wa Uwanja wa Munispaa ya Mombasa. Kwanza, ningependa kuwashukuru Maseneta wote ambao waliweza kuchangia Hoja hii: Sen. Madzayo, ambaye aliunga mkono wa kwanza, Sen. Maanzo, Sen. Cherarkey, Sen. Olekina, Sen. (Dr.) Khalwale, Sen. Beth Syengo, Sen. Mungatana, Sen. Omogeni, Sen. Oketch Gicheru, na mwisho, Sen. Mandago, ambao walichangia kwa lugha ya Kitaifa ya Kiswahili. Jambo la kufurahisha ni kwamba Hoja hii tumeizungumzia na kuichangia kwa lugha ya Kitaifa ya Kiswahili. Ni mara ya kwanza kwa Hoja kuletwa katika Bunge hili kwa lugha ya Kiswahili na kujadiliwa kwa Lugha ya Kiswahili mpaka ikakamilika. Ningependa pia kushukuru mchango wa Maseneta wote ambao wamechangia Hoja hii. Wamesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa uwanja wa kimataifa katika eneo ya Mombasa. Kwa mfano, sasa hivi, uwanja unaotumika wa Shirika la Bandari (KPA), lakini kwa sasa, wameufunga kwa sababu wanaufanyia marekebisho. Uwanja mwingine ambao unaweza kutumika na timu ya Bandari ni Uwanja wa Ukunda na Ukunda ni karibu kilomita 40 kutoka Jiji la Mombasa. Hali hii inaonyesha kwamba ipo dharura ya kukamilishwa kwa uwanja huu ili watu waweze kupata nafasi ya kuona michezo ya kimataifa. Vile vile, kushughulika na maswala mengine kwa sababu, uwanja sio wa mpira peke yake, lakina uwanja huu utakuwa na kidimbwi cha kuogelea, hall (auditorium) ya Sanaa. Kwa hivyo, ni uwanja ambao ni kamili kabisa. Swala lingine ni kwamba, sio kwamba Kaunti ya Mombasa haijaegeza hakika uwanja huu, lakini pesa zile ambazo wanaegeza kwa mfano katika bajeti ya mwaka 2023/24 waliweka Kshs80 milioni peke yake. Shilingi milioni 80 hazitoshi jambo lolote. Milioni 80 inatakikana zilipe askari wanaolinda pale na pia kulipia usafi katika uwanja ule. Hizo ni pesa ambazo itachukua zaidi ya miaka kumi au 20 kukamilisha ujenzi wa uwanja ule. Ningependa pia kuguzia maswala ambayo Sen. (Dr.) Khalwale ameyaguzia hapa kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa pesa Kshs500 milioni. Hakuna ushahidi wowote kuonyesha ya kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa fedha zikijumuisha kufikia Kshs500 milioni. Kwa sasa, Serikali kuu imepeleka wahandisi kutoka kwa Idara ya Public Works kuangalia na kutathmini ile kazi ambayo imefanyika pale. Wahandisi hawa wote wametoa ripoti ya kwamba kwa sasa hakuna pesa ambazo zimeweza kufujwa. Kwa hivyi, sio kweli kama alivyosema Sen. (Dr.) Khalwale wakati alipotoa machango wake mara ya kwanza na leo pia alipokuwa akiendelea kutoa mchango wake kusema kwamba kulikuwa na ubadhirifu wa zaidi ya Kshs500 milioni. Ripoti zote za Mhasibu Mkuu, yaani Auditor-General, ambazo zimekuja katika Bunge hili, hakuna ripoti yoyote ambayo imesema ya kwamba kuna pesa Kshs500 milioni ambazo zimepotea katika uwanja wa Manispaa ya Mombasa. Kama Sen. (Dr.) Khalwale ana ripoti hiyo, kesho ailete katika Bunge hii ili tuiangalie na tuone kama pesa hizo zimebadhirishwa, basi tutaondoa Hoja hii ili kwanza tuangalie maswala ya pesa zilizopotea kabla ya kurudi hapa."},{"id":1419259,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419259/?format=json","text_counter":311,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1419260,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1419260/?format=json","text_counter":312,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Mchango mwingine umetoka kwa Sen. Mungatana. Unajua siku zote jicho linaona lakini jicho pia huingia kitakataka. Nashangaa Sen. Mungatana anazungumzia maswala ya Mombasa akisema kuwa tuangalie tusifuje pesa za serikali. Lakini tukiangalia Kaunti ya Tana River, haina hata uwanja wa stadium. Huu ni mchango ambao sio wa Mombasa pekee, lakini Pwani nzima. Uwanja huu utafaidi timu kutoka Tana River, Lamu, Kilifi---"}]}