{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=148007","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=148005","results":[{"id":1498252,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498252/?format=json","text_counter":412,"type":"speech","speaker_name":"Jomvu, ODM","speaker_title":"Hon. Twalib Bady","speaker":null,"content":" Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii nichangie Mswada huu wa 35 wa 2024, juu ya utaratibu wa uokotaji wa ushuru katika gatuzi zetu (County Governments (Revenue Raising Process) Bill (National Assembly Bill No.11 of 2023). Mhe. Spika wa Muda, naunga mkono kwanza kwa kusema kuwa hali hii sio hali mbaya. Hii ni hali itakayoweza kutusaidia ili kuona kuwa sio wote katika gatuzi zetu wana uwezo wa kuamka siku moja na kusema kwamba wanataka kutoa ushuru wa jambo hili au lile. Kwa hivyo, naona Mswada huu utaweza kuthibiti zile kaunti juu ya jambo gani ambalo linatakikana kutolewa ushuru, na litamfaidi vipi wananchi. Vile vile, kwenye jambo hili, kuna wale Madiwani wa mara ya Kwanza, yaani first"},{"id":1498253,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498253/?format=json","text_counter":413,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"timers"},{"id":1498254,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498254/?format=json","text_counter":414,"type":"speech","speaker_name":"Jomvu, ODM","speaker_title":"Hon. Twalib Bady","speaker":null,"content":", ambao katika kila gatuzi, kuna sheria zake ambazo zinaitwa bylaws . Vile vile, hao madiwani kuona kwamba zile bylaws zikipitishwa, zisiwaumize mwananchi ambaye anamwakilisha katika sehemu yake. Lakini kuna mambo ambayo nitatofautiana kidogo na ndugu yangu, Mhe. Owen Baya, ambaye amenitaja kwa jina, na vile vile akamtaja Mhe. Kimani Ichung’wah. Amesema kuwa tulikuwa katika forum moja ya Port users, na tukasema kuwa jambo hili la kuwatoza watu ushuru kila mahali linafanya biashara iwe ngumu hapa Kenya. Ningetaka kumwambia ndugu yangu, Mhe. Owen, kuwa sisi kama County Government ya Mombasa, mpaka leo, bado tuna- demand na kusema kuwa ni haki yetu kupata ushuru unaotoka katika Bandari ya Mombasa. Kule Marekani, kuna bandari inayoitwa Long Beach, inayozalisha mapato kwa"},{"id":1498255,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498255/?format=json","text_counter":415,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"municipality"},{"id":1498256,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498256/?format=json","text_counter":416,"type":"speech","speaker_name":"Jomvu, ODM","speaker_title":"Hon. Twalib Bady","speaker":null,"content":"ya pale. Kule Afrika Kusini, kuna bandari inayoitwa Durban Port. Municipality yao inayoitwa Thekwini inazalisha mapato kutokana na Durban Port. Ukiangalia mahali kama Port of Antwerp, watu wanalipa ili watumie Port hiyo. Kwa hivyo, Port City ya Mombasa ina haki ya kupata ushuru kama vile nchi nyingine zinapata ushuru kutokana na port cities katika sehemu zao."},{"id":1498257,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498257/?format=json","text_counter":417,"type":"speech","speaker_name":"Jomvu, ODM","speaker_title":"Hon. Twalib Bady","speaker":null,"content":"Kitu ambacho Mhe. Owen amekitaja na nataka nikirekebishe, ni kuwa container ikiletwa, watu huwa wanatozwa ushuru mara mbili. Hii ni double charge. Mojawapo ya hizo"},{"id":1498258,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498258/?format=json","text_counter":418,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"charges"},{"id":1498259,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498259/?format=json","text_counter":419,"type":"speech","speaker_name":"Jomvu, ODM","speaker_title":"Hon. Twalib Bady","speaker":null,"content":"ni Terminal Handling Charge, ambayo ni ya kuanua mizigo. Inalipwa kwa the KenyaPorts Authority (KPA). Vile vile, katika shipping line, kuna charge nyingine inayoitwa"},{"id":1498260,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498260/?format=json","text_counter":420,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Delivery Order Fee"},{"id":1498261,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1498261/?format=json","text_counter":421,"type":"speech","speaker_name":"Jomvu, ODM","speaker_title":"Hon. Twalib Bady","speaker":null,"content":". Ukileta container, unapewa Bill of Lading, inayomaanisha kuwa wewe ndiye mmiliki halisi wa container hiyo. Ukifika katika shipping line, una- surrender Bill ofLading and in return, unapewa Delivery Order kwa bei ya USD $80. Hayo ndiyo mambo yanayofanya gharama ya kufanya biashara kuwa juu. Ndio maana leo hii tumepoteza biashara tuliyokuwa nayo kutoka Goma, Butembo, Kinshasa, Lubumbashi, Kampala na Rwanda. Wengi wao wanakimbilia Bandari ya Dar-es-Salaam kwa sababu Bandari hiyo imeondoa TerminalHandling Charges (THC) na Delivery Order Fee. Mtu akipeleka Bill of Lading yake, inajulikana kuwa hiyo ni mali yake."}]}