{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=148382","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=148380","results":[{"id":1502002,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502002/?format=json","text_counter":204,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Munyi Mundigi","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Asante Bw. Spika wa Muda kwa kuniruhusu nichangie Hoja ya Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Kenya iliyokuwa siku ya Alhamisi katika Bunge La Taifa. Shughuli hii iliwaleta pamoja Maseneta na Wajumbe wa Bunge la Taifa. Naunga mkono Hotuba ya Rais kwa sababu iligusia masuala ya kilimo ambapo mimi ndiye naibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Alizungumzia suala hili kwa urefu. Nakumbuka vyema Serikali ya Kenya Kwanza iliposhika hatamu, mbolea ilikuwa inauzwa Shilingi 6,500 za Kenya. Wakati huu wa kipindi cha miaka miwili, mbolea hii hii sasa inauzwa shilingi 2,500 za Kenya ili mwananchi awe na pesa mfukoni. Masuala ya kilimo ni njia moja ya kuchangia uchumi wa Kenya. Wakulima wengi wanaofanya ukulima wa kahawa, majani chai, makadamia, miraa, muguka, pamba, miwa katika sehemu za Bonde la Ufa na maembe, wote wanahitaji mbolea. Inafaa kaunti zote 47 zijengewe mabwawa ili kilimo kiweze kundelea vilivyo. Niko na imani Rais atatimiza. Tunapendekeza bei ya maziwa iwe shilingi hamsini na wakulima husika walipwe kwa kipindi cha mwezi mmoja. Biblia husema, mko na macho na hamuoni, na mko na masikio wala hamsikii. Tukiangalia majani chai, kila mtu anasheherekea kwa sababu kilimo hiki kinaleta faida ambayo haijashudiwa kwa vipindi vya awali. Vile vile, bei ya kahawa imeenda juu. Vile vile Rais alipendekeza kilimo kiwe cha kuongeza dhamana ili mambo yote ya ukulima yarudi mashinani kwa kaunti zetu zote kama inavyotakikana kwa mfumo huu wa ugatuzi. Ningeomba Seneti tumuunge mkono Rais kwa kipindi hiki. Aidha, Rais alizungumzia masuala ya waalimu. Ukilinganisha kipindi cha awamu cha Rais Mstaafu na awamu hii ya Rais aliye mamlakani, kwa muda wa miaka miwili, Serikali ya Kenya Kwanza imeajiri waalimu 56,000 na ameahidi kuongozea wengine. Hivyo basi, naomba tumuunge mkono kwa azma yake ya kuboresha elimu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1502003,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502003/?format=json","text_counter":205,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Munyi Mundigi","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ni kweli kuna shida ya shule za vyuo vikuu na inafaa iangaliwe. Pia, Serikali haina wafanyikazi wa kwenda mashinani kuhamasisha watu kuhusu miradi ya Serikali ambayo Rais amekuwa akizindua mara kwa mara. Rais pia alizungumzia suala na halmashauri ya Social Health Authority (SHA) ambayo inasimamia Bima ya Afya ya Jamii almaarufu Social Health Insurance Fund (SHIF). Ombi langu ni tuiunge mkono Serikali ya Kenya Kwanza. Sisi wafanyikazi wote tunateseka na kuumia kwa kutozwa pesa. Baadhi yetu tunatozwa shilingi 20,000 na hata wengine 30,000. Hata hivyo, tunaelezwa kuwa itakapoanza kufanya sawasawa, watu wote wanaougua saratani na magonjwa mengine kama vile kifua kikuu yatashughulikiwa. Magonjwa hayo yametusumbua sana kama Wajumbe kwa kufanya michango ya kila mara kule mashinani itaisha. Mpango huu ukifaulu wagonjwa hao wote hawatakuwa walikipa pesa. Kama Seneta wa Kaunti ya Embu naomba niongezee kwa kusema hivi. Serikali ya hayati Rais Kibaki ilisema kuwa kila mtu akifisha miaka sabini awe akipata msaada wa pesa fulani. Serikali ya rais mstaafu Uhuru Kenyatta haikuongezea idadi ya walengwa. Katika Serikali ya Kenya Kwanza mtu mwenye miaka sabini na kuendelea anapata pesa kila mwezi. Kama tukimshikilia rais, tunaona Serikali yake inaendelea kwa njia inayofaa. Wanaofanya kazi ya Community Health Promoters kule vijijini wanalipwa shilingi 5,000. Hata hivyo kuna matatizo kwa sababu Wabunge wa Bunge la Kitaifa wanakataa kuidhinisha pesa kwa kaunti. Nawarai Wajumbe wa Mbunge la Taifa watuongezee zile pesa ili Community Health Promoters walioajiriwa na Serikali ya Kenya Kwanza waweze kupata mishahara. Rais pia aliguzia suala la Adani Group. Naomba niwajuze Seneta wa Nairobi, Sen. Maanzo wa Kaunti ya Makueni na Seneta wa Kitui ambaye ni Bishop kwamba tuunge mkono Serikali ya Kenya Kwanza ili ifanye kazi inayofaa. Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Siku ya Hotuba, Rais pia alifutilia mbali kandarasi ya Uwanja Wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na ile ya Kampuni ya Usambazaji Umeme Nchini (KeTRACO). Pia aliahidi mambo uya procurement yatakuwa katika mtambo wa e-Citizen. Hivyo basi, sio lazima kila siku tuwe ni kupigana hapa na pale. Naomba tuiunge mkono Serikali kwani hata hali ya uchumi imeimarika. Rais aliambia Taifa ya kwamba, alipochukua hatamu mambo ya i nflation illikuwa nine per cent na sasa ni 2.7 per cent. Tuugangeni pamoja kwani umoja ni nguvu. Serikali hii iko na maono angalau tuone tutamiliza muhula huu vipi. Sio kila wakati ni kupiga Serikali. Kwa suala la Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC), nakumbuka mwaka jana kama Serikali ya Kenya Kwanza tulipitisha majina saba. Baadaye, ikasemekana lazima upande wa Mrengo wa Walio Wachache Bungeni wa Azimio na wengine sharti waongezee watu wawili. Hii ndiyo imeleta shida. Kwa hivyo, naomba Maseneta wote tuungane pamoja ili tushikilie serikali ya Kenya Kwanza. Tukifanya hivyo, mapato ya Serikali ya Kitaifa na yale ya kaunti 47 yataimarika. Bw. Spika wa Muda, ni mimi Seneta wa Kaunti ya Embu, Daktari Alexander Munyi Mundigi. Naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1502004,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502004/?format=json","text_counter":206,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"Asante Bw. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Hotuba ya Rais ya Hali Halisi ya Taifa iliyotolewa mnano tarehe 21.11.2024 kuambatana na Kifungu Cha 132(1) ( C) cha Katiba yetu. Ninampongeza Rais kwa kutekeleza jukumu hili la kikatiba ambalo ni muhimu sana la kujuza Bunge kwa mujibu wa Katiba. Bw. Spika wa Muda, ni masikitiko kwamba katika Hotuba yake, Rais hakuzungumzia maswala ya ugatuzi. Hotuba yake yote haikugusia maswala ya serikali za kaunti ambazo ni kiungo muhimu katika nchi yetu. Ikumbukwe kwamba tulikuwa na mvutano kuhusu Division of Revenue Bill ambapo mpaka wiki iliyopita ndipo Kamati ya Uwiano iliweza kukubaliana kuhusu kiwango cha pesa zitakazokwenda kwa kaunti zetu. Tangu mwezi wa saba hadi wa kumi mwaka huu, kiwango cha fedha za kaunti kilikuwa hakijulikani. Kwa hivyo, kulikuwa na shida ya kaunti zetu kupata pesa kutoka kwa Hazina Kuu ya Kitaifa. Ijapokuwa sheria inatoa fursa kwa Hazina Kuu ya Kitaifa kulipa mpaka nusu ya pesa ambazo zilipelekwa katika kaunti zetu mwaka uliotangulia, Serikali imekuwa na shida ya kutuma pesa, hivyo basi kuziweka serikali za magatuzi katika nchi yetu katika hali ngumu ya kulipa madeni na kulipia huduma ambazo wanatoa katika kaunti tofauti tofauti. Pesa zilitumwa katika kaunti zetu wiki mbili zilizopita. Hata hivyo, kaunti nyingi zimepata hasara kwa sababu ilibidi wakope pesa kwa riba ya juu ili walipe mishahara na huduma nyingine. Jambo la pili ambalo limenisikitisha ni hali ya haki za binadamu katika nchi yetu. Wakati wa maandamano ya Gen Z, vijana wengi walipigwa risasi na kuuawa kiholela. Ijapokuwa Rais alitoa hakikisho kwamba wale wote ambao waliua bila hatia watachukuliwa hatua, mpaka sasa, hatujaona jambo lolote ambalo limefanyika kutekeleza matamshi hayo ya Rais na vile vile kuhakikishia familia za wale ambao waliondoka kwamba haki itatendendeka kuhusiana na watoto na jamaa wao. Jambo lingine la kusikitisha pia ni kwamba maswala ya utekajinyara yamezidi katika nchi yetu. Cha hivi karibuni ni kisa ambacho watu wanne wa asili ya Kituruki walitekwa nyara hapa Nairobi na kupelekwa Turkey bila familia zao kujulishwa wala sheria kufuatwa. Sheria yetu inasema kuwa iwapo mhalifu yuko hapa na anatakikana katika nchi nyingine na kuna makubaliano kati ya nchi yetu na nchi anayotakikana kupelekwa kortini, anafaa kufanyiwa kesi ya uhamisho kabla ya kwenda kushtakiwa kuhusu makosa aliyofanya kule. Licha ya kuwa na sheria, watu wale walirejeshwa Istanbul kule Uturuki ili kushtakiwa kwa makosa ambayo hayajulikani. Ikumbukwe kuwa walikuwa wahamiaji halali katika nchi yetu ya Kenya. Ina maana kwamba mhamiaji yeyote hayuko salama katika nchi aliyohamia. Mwingine aliyechukuliwa wiki mbili zilizopita ni Kiongozi wa Upinzani kule Uganda, (Dr.) Kizza Besigye. Alichukuliwa hapa Nairobi katika hali hiyo. Utekajinyara na mauaji ya kiholela, ama extrajudicial killings, ni mambo ambayo Rais alifaa kuzungumzia kwa undani zaidi kwa sababu ni mambo ambayo yanahusiana na usalama wa Wakenya. Hata mimi binafsi sina usalama kwa sababu watu wanatekwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1502005,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502005/?format=json","text_counter":207,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Faki","speaker_title":"","speaker":{"id":13211,"legal_name":"Mohamed Faki Mwinyihaji","slug":"mohamed-faki-mwinyihaji-2"},"content":"nyara na mwishowe kupatikana wameuawa. Wengi wa waliouawa ni vijana ambao walishiriki katika maandamano ya Gen Z. Vile vile, tulitarajia Rais kuzungumzia tuhuma ambazo Gen Z walikuwa nazo wakati walipokuwa wanaandamana hadi kwenye Bunge hili mwezi wa sita mwaka huu. Hata hivyo, Rais hakugusia hayo. Kwa hivyo, ni wazi kwamba Rais pamoja na washauri wake hawasikii wala kufuata mambo mengi ambayo yanaathiri Wakenya. Ijapokuwa Kenya yetu ni democrasia, maswala ya mauaji ya kiholela, utekajinyara, na ukandamizaji wa haki za kibinadamu kupitia mambo kama vile mauji na mengineyo yanatia doa nchi yetu kwa sababu Kenya ni mwanachama wa Community ofNations . Tumetia sahihi kwenye mikataba mingi kuhusu kuwalinda wahamiaji na haki za kibinadamu. Tumetia sahihi mikataba mingine mingi ambayo hatuwezi kupuuza kwa sababu sisi tumekubalika katika Community of Nations . Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, Hotuba hiyo haikukamilika kwa sababu mambo ambayo tumezungumzia ni muhimu na yalifaa kuangaziwa na Rais katika Hotuba yake."},{"id":1502006,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502006/?format=json","text_counter":208,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Sen Tabitha Mutinda, you have the Floor."},{"id":1502007,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502007/?format=json","text_counter":209,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Tabitha Mutinda","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Mr. Temporary Speaker, Sir, I rise to appreciate the President for his precise, timely and direct to point Address to the nation last week on Thursday. Let me start by appreciating his Address on the issue of femicide. As women leaders, we were delighted when this subject matter was addressed at his level because it is a national crisis. It is an issue that we condemn strongly. I also wish Florence Wanjiku quick recovery. She is currently recovering at a Nakuru hospital after the heinous actions by Elias. These are issues that even the President condemns highly. I want to appreciate the fact that he directed that there be Gender-Based Violence (GBV) desks at the county or grassroots level where women can quickly get responsive services, unlike having the desks situated at the police stations. It has been a challenge such that when such incidents occur, it becomes a challenge for women to come out to address because they appear as if they are just domestic matters. Now that desks will be at the grassroots, it will give a wider coverage as far as issues of femicide are concerned in this country. He also talked about different parenting as far as the boy-child is concerned. Let them be strengthened, so that even when it comes to societal and family matters, the boy child grows to become more responsible. These issues that we are seeing coming from men will be reduced in the future and that is what we pray for. So, we appreciate him for that. There was also the issue of cancellation of the Adani deal. You will all remember that when the issue of Adani came out, there were so many concerns, especially from our brothers and sisters working for the Kenya Airports Authority (KAA). They said they were not comfortable with that kind of agreement because they did not understand it. The cancellation of the agreement is an indication that the President listens to the people. University students raised concerns about the Education Funding Model that has been implemented. The President took time, called for a county hall meeting, and had a The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1502008,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502008/?format=json","text_counter":210,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Tabitha Mutinda","speaker_title":"","speaker":null,"content":"conversation with “comrades” from different universities in this country. That is another indication that he listens to the people. If you can remember, a few months ago when Parliament was invaded because of the Finance Bill, 2024, the President did not assent to it. That is still an indication that he is a listening President, but there have been concerns on whether he is listening. The cancellation of Adani deals last week by His Excellency the President is total evidence that he is a listening President and will continue to listen so that the issues Kenyans raised can be addressed in a better way. As a country, it is high time we embraced the Public Private Partnership (PPP) system. Looking at our financial status, the recurrent expenditure is very high and we need the PPPs so as to develop the infrastructure that is going to improve our economy, moving forward. Mr. Temporary Speaker, Sir, His Excellency the President touched on the issue of the teachers in his Address. We are very happy because this year alone, over 56,000 teachers have been employed in our country cutting across, which improves our education system. There is also a plan to recruit 20,000 teachers next year in January. This process is ongoing. Within these two years, we will be achieving 76,000 teachers’ employment, which has not happened in the past years. This is a big stride. A stable education system will ensure that the issues of concern raised by our young people are addressed. He also talked about the agricultural sector. The cost of fertiliser has gone down to Kshs2,500. There is a VAT cut cost on the raw materials for production, like pesticides, which narrows the cost of production for our produce for the end-user. Lowering the cost of these products also lowers the commodity price. For example, the cost of unga, hence we achieve food security. The lowering of cost on the raw materials for production is the reason that has brought the cost of production down. Lowering the cost of fertilisers played a very key role. This has a very big impact to us as a country. His Excellency the President also talked about Taifa Care with a lot of passion. Both Houses passed this Bill; the Universal Health Care Bill. The Social Health Insurance Fund (SHIF) broadly takes care of emergencies. In the past, when someone got an accident, some Kenyans have been lenient enough to assist. However, there are some who have not. The reason has been that when you get them to hospital, who will take care of the bill. However, right now, SHIF takes care of such emergencies. If you take a patient with an emergency case to the hospital, SHIF requires that the patients be given medical care. It also takes care of the outpatient and inpatient that the National Health Insurance Fund (NHIF) too did. Further to that, it takes care of chronic diseases, for example, cancer. People have done contributions to travel out of the country to get specialized medical care. This is a very expensive affair, financially. It has drained families. People have lost their loved ones because they have to travel out of the country to get adequate medical attention, which is very expensive. With SHIF in place, it is taking care of chronic diseases. There is also a Facility Improvement Fund (FIF) for maintenance of equipment in hospitals. Facilities are going to be up to date and people will no longer be told that the machines have a challenge and they cannot get medical tests. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1502009,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502009/?format=json","text_counter":211,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Tabitha Mutinda","speaker_title":"","speaker":null,"content":"The Fund will also ensure that equipment in different hospitals is maintained to the best of standards. There is also an opportunity for the hospitals to acquire modern machines that are up to date and are able to take care of the modern technology that is in place. With regard to technology, His Excellency the President talked about the issue of digitization of Government services. When we started, we had about 300 digital services in this country. However, that has increased to about 25,000 e-services. We look forward to achieving at least 99 or 100 per cent Government entities, offering their services digitally. I speak as the ambassador of the International Certificate of Digital Literacy (ICDL). I am a champion of digital literacy. We have also seen an aspect of digital literacy in the constituencies through the Members of Parliament (MPs), who have set up digital hubs. They not only create jobs, but ensure that the services that the Government is offering are spread across the country. As I conclude, His Excellency the President talked about the protests. The Constitution is very clear that protests are allowed, but they need to be peaceful. Demonstrations and picketing should be very peaceful. The President did not say that only a specific group or---"},{"id":1502010,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502010/?format=json","text_counter":212,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Wakili Sigei","speaker_title":"The Temporary Speaker","speaker":null,"content":" Sen. Madzayo, proceed."},{"id":1502011,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502011/?format=json","text_counter":213,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"The Senate Minority Leader","speaker":{"id":679,"legal_name":"Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo","slug":"stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"},"content":" Asante sana Bw. Spika wa Muda. Kwanza, nampa kongole Rais kwa kutoa Hotuba yake ya hali halisi ya nchi ya Kenya ya mwaka huu. Sikudhani angefanya hivyo kwa sababu siku zilikuwa zimeyoyoma na mwaka unaenda kuisha. Kalenda ya Bunge ilikuwa imefika mwisho, kwani tumebaki na siku saba ili Bunge liende kwa likizo. Lakini ni vyema alikuja kutoa Hotuba ya hali halisi ya Taifa ya mwaka wa 2024. Kitu cha muhimu katika Hotuba ya Rais ni kugusia mambo mbalimbali ya muhimu ambayo wananchi wa Kenya wangependa kusikia na kuona suluhisho limepatikana. Bw. Spika wa Muda, katika Hotuba ambayo Rais alitoa, hakuweza kugusia kitu cha muhimu kilichotendeka mwaka huu katika maeneo yetu ya Bunge, ilhali alitoa Hotuba hiyo akiwa Bunge. Kitendo cha muhimu kilichotendeka Bungeni ni kuuawa kwa vijana wa kike na kiume katika barabara tofauti hapa Nairobi. Wengi walipoteza maisha yao katika maeneo ya Bunge. Kwa hivyo, ilikuwa ni muhimu kwa Raisi kutaja mambo hayo akitoa Hotuba yake ya 2024 akiwa ndani ya Bunge, mahali ambapo vijana wadogo; Generation Z, walipigwa risasi na polisi wetu na wakafa. Hatuwezi kusema ni wangapi, lakini waliokufa na kupata majeraha na walio hospitalini hadi sasa ni wengi. Kuna wengi waliokufa na hawakupatikana na wazazi wao bado wanawatafuta, kwani hawajui waliko. Ilikuwa ni muhimu aeleze Wakenya kinaga ubaga katika Hotuba yake watoto waliopotea wako wapi. Je, waliopata majeraha wamepata matibabu? Je, gharama ya waliopata majeraha na kuenda hospitali kutibiwa zimelipwa? Je, Serikali imechukua hatua gani kwa waliopoteza maisha yao, ikiwa Bunge limepitisha Hoja ya kwamba waliopoteza maisha na walioumia walipwe kulingana na maumivu yao au hela waliotumia kuzika wapendwa wao. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."}]}