{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=148456","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=148454","results":[{"id":1502742,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502742/?format=json","text_counter":174,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"Bw. Spika wa Muda, huu ni wakati wangu wa kwanza kutoa maoni yangu kuhusu sheria hii ambayo tumetunga juzi kuhusu makadirio ya fedha kwenye Serikali Kuu na zile za kaunti. Nilipokuwa nikichangia kwenye Kamati ya Usuluhishi, nilikuwa mmoja wa wale wabunge wa Seneti ambao walikataa. Maoni yangu ni kuwa zile pesa ambazo kaunti zilikuwa zimepewa, zilikuwa zimetosha na hakukuwa na haja ya kuziondoa kwa sababu zile pesa ambazo Serikali Kuu inazitumia kiasi chake ni kikubwa kwani ni asilimia 85. Tafadhali hakikisha ugatue yale majukumu ambayo gatuzi zote zinapaswa kufanya na hela zao mwaka ujao. Sasa tumefanya uangalizi wetu. Tumekagua vitabu vyote vya kaunti zote 47. Sasa tumefika mwaka wa 2023/2024. Kwa Kimombo tunasema tuko"},{"id":1502743,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502743/?format=json","text_counter":175,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"current."},{"id":1502744,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502744/?format=json","text_counter":176,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"Tunafanya hivi kwa sababu katika gatuzi zetu ndiko umaskini mwingi uko. Watu wengi wanaishi kwa kaunti zetu. Hivyo basi, huko mashinani ndiko tunahitaji barabara nyingi, maji, ukulima na madaktari. Jambo la kwanza ambalo sisi kama Seneti tunapaswa kufanya ni kuhakikisha tumemuuliza Rais kwa heshima ahakikishe kuwa amegatua fedha na yale majukumu ambayo yamegawiwa kaunti. Pili, magavana wamekuwa wakisema kila wakati kuwa hawajapata pesa kutoka kwa Serikali na pia mishahara haijawafikia. Lakini, tungependa kuwaambia ndugu zetu magavana kuwa Wakenya sio wajinga sasa. Wakenya wanajua ni wakati gani Serikali inatoa pesa na wakati ambao fedha hizi hufika kwa gatuzi zetu mashinani. Magavana wanapopata hizi pesa wanatakiwa kuzitumia vizuri ili zifanye kazi. Ninapozungumza sasa hivi, kwa Hazina ya Fedha ya Kaunti County Revenue"},{"id":1502745,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502745/?format=json","text_counter":177,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Fund (CRF)"},{"id":1502746,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502746/?format=json","text_counter":178,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"katika Kaunti yangu ya Kisii, kuna shillingi bilioni tisa na laki tatu. Lakini, Gavana wangu amekuwa akiambia watu hakuna pesa. Waliokuwa wakandarasi hawajalipwa, wafanyikazi wa kaunti wanafutwa kazi na wengine kuajiriwa. Hakuna mambo yanaendelea. Hakuna barabara na mvua kwa sasa imenyesha. Ukiangalia zile shida ziko kwa kaunti zote kama vile Sen. Cherarkey alikuwa anasema, kwa heshima utamwambia Gavana wako ya kwamba pesa mimi ndimi nimeuliza, nikazichunga, zikaja na sasa ziko kwa account . Tafadhali, tumia hizi pesa usaidie watu wetu. Ukifanya hivyo, anakutafutia goons . Wanakuja na panga na wengine na bunduki. Ooh, huyo Seneta anataka kutunyang’anya ugavana wetu, ooh, huyo Seneta ndiye mwizi. Ningependa kuambia magavana wetu hatuna vita na wao. Wengine wetu hata hatutaki kuwa magavana. Kaunti yangu ya Kisii napata kila mwaka shilingi bilioni kumi na tano. Kwa miaka miwili Kisii imepata bilioni thelathini. Ukitoa pesa za mishahara shilingi bilioni sita na nusu, bilioni kumi na tatu ndizo zimeenda kwa mishahara. Shilingi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1502747,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502747/?format=json","text_counter":179,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"zingine bilioni kumi na sita ama kumi na mbili ndizo hubaki za kuwafanyia wananchi kazi. Hamna madawa hospitalini, miradi iliyokuwa inaendelea ya maji haifanyiki, pesa zote zinazotoka kwa donors zimesimamishwa katika Kaunti ya Kisii, kwa sababu vigezo vyote ambavyo vimekwa na wafadhili vimekiukwa. Gavana alipoingia huko alitoa wale waliokuwa wakitia signature na kuweka watu wake. Hakujua sheria inasema hawezi kufanya hivyo. Ukiuliza walimu wa shule za chekechea, hawajalipwa mishahara. Wengine mishahara yao ni minimum wage . Utamuajiri aje mtu afunze mtoto wako kutoka darasa la kwanza hadi la tatu au la nne, ilhali unamlipa shilingi elfu saba? Huyu ni mtu amesoma na hata wengine hadi chuo kikuu. Wale Community Health Promoters (CHPs) wa vijijini Serikali iliahidi kutenga pesa watakazokuwa wanapata. Je, nini kimefanyika? Katika Kaunti ya Kisii, CPHs hawajalipwa ilhali kwa county revenue fund ya Kisii, kuna shilingi bilioni sita. Sasa hizi ndizo shida zetu hapa Kenya. Kuna ufisadi, wizi na lack of management . Bw. Spika wa Muda, tunapaswa kujiuliza kama Wakenya swali hili. Iwapo mtu anataka kuwa gavana, anafaa kwenda shule gani kwa sababu kazi imeshinda wengi wao? Mtu akichaguliwa kuwa gavana, kazi ya kwanza ni kuwafuta kazi watu walioajiriwa na gavana aliyemtangulia kwa sababu si wa ukoo wake. Anavunja sheria kwa kuajiri watu wa ukoo wake kwa sababu walimpigia kura. Hiyo ni njia ya kuwaambia kuwa yeye ni mzuri lakini gavana aliyemtangulia alikuwa mbaya. Watu hao wote ni Wakisii. Wote ni Wakenya na wanalipa ushuru. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo yanatukera. Tumefika mahali ambapo lazima tujiulize kama Wakenya. Je, tutalinda vipi pesa ambazo wananchi wa Kenya wanatoa kupitia kwa ushuru? Namheshimu sana Gavana wa Kakamega. Nilikuwa katika mkutano huo na sikutaka kujibu. Alisema kuwa the Controller of Budget (CoB) ndiye anamnyima pesa. Ni kweli kuwa baadhi ya magavana wamekatazwa kutoa pesa na Msimamizi wa Bajeti. Vile Sen. Cherarkey alivyosema, wakiwa na CIDPs, wanaweza kutumia"},{"id":1502748,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502748/?format=json","text_counter":180,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Integrated Financial Management Information System (IFMIS)"},{"id":1502749,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502749/?format=json","text_counter":181,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":". Baada ya kuingiza ujumbe katika IFMIS, CoB na Ministry of Finance and Economic Planning wanafanya"},{"id":1502750,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502750/?format=json","text_counter":182,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"entry,"},{"id":1502751,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1502751/?format=json","text_counter":183,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Onyonka","speaker_title":"","speaker":{"id":13592,"legal_name":"Onyonka Richard Momoima","slug":"onyonka-richard-momoima"},"content":"kisha wataeleza kazi aliyofanya yule anayetaka kulipwa. Vile vile, wataeleza"}]}