{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=150339","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=150337","results":[{"id":1521572,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521572/?format=json","text_counter":132,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Sifuna","speaker_title":"","speaker":{"id":13599,"legal_name":"Sifuna Edwin Watenya","slug":"sifuna-edwin-watenya"},"content":"Mhe. Spika, kwanza ningependa kumkosoa Kiongozi wa Walio Wengi kwamba haijachukua siku zaidi ya kumi tangu tumzike Mhe. Leonard Mambo Mbotela. Tulimlaza pale Langata tarehe 15 mwezi huu. Najua Kiongozi wa Walio Wengi labda hiyo tarehe inakuchanganya kwa sababu ulikuwa katika maeneo ya Addis Ababa kwa shughuli ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa African Union Commission (AUC). Mnavyojua, mimi ni mtu wa mkono wa Mhe. Raila Odinga. Kwa hivyo, nilisalia hapa na tukajiunga pamoja na mwakilishi wa kina mama wa Kaunti ya Jiji Kuu la Nairobi, Mhe. Esther Passaris, pamoja na familia ya Mwenda zake Leonard Mambo Mbotela katika maombi pale All Saints Cathedral. Ilikuwa ni siku ambayo sote tulimkumbuka huyu shujaa wa utangazaji wa habari katika taifa letu la Kenya. Bw. Spika, kinachonishangaza ni kwamba unakuta Seneta kama Sen. Cherarkey anatumia fursa hii ambayo tunamuenzi mtangazaji mkuu katika taifa letu kuwakosoa waandishi wa habari. Mhe. Spika, habari unazochagua kuona ni u pto you, y aani, ni wewe utachagua ile channel utataka kwa sababu tulipokuwa tunakua, kulikuwa na kituo kimoja cha matangazo ambacho kilikuwa cha mama na baba. Wakati huu kuna vituo vingi. Ikiwa unaona kuna kimoja ambacho habari zake zinakukera, uko huru wa kubadilisha mitabendi, kama walivyokuwa wakisema. Bw. Spika, ninavyojua ni kwamba, stesheni za kutangaza zitatangaza matukio jinsi ambavyo yalifanyika. Kwa mfano, leo Sifuna alirushwa nje ya Bunge la Seneti. Hautarajii kwamba waseme hakurushwa nje. Kwa hivyo, tuvipe vyombo vyetu vya matangazo nguvu ya kufanya kazi zao. Bw. Spika, tulikuwa na pendekezo mwaka wa 2007 kwamba tuwe na Heroes Corner katika kiwanja chetu cha Uhuru Gardens. Nimesema hapa mara nyingi kwamba kiwanja hicho kilitwaliwa na jeshi na mpaka sasa hatujaweza kufanya kazi hiyo ya kuweka Heroes Corner pale. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1521573,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521573/?format=json","text_counter":133,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Sifuna","speaker_title":"","speaker":{"id":13599,"legal_name":"Sifuna Edwin Watenya","slug":"sifuna-edwin-watenya"},"content":"Kuna sharia inayojulikana kama Kenya Heroes Act. Sheria hii inasema kwamba tuwatunze na kutoa njia ya kuwatunza hawa mashujaa wetu. Nilishtuka sana kuona Spika mwenzako katika Bunge la Kitaifa akisema ameshangazwa na kusikia kwamba Leonard mambo amezikwa katika makaburi ya Langata. Bw. Spika, sheria hiyo inataka Bunge, yaani sisi, tutoe fedha ili kuwasaidia hawa mashujaa wetu. Hamna mtu mwingine mwenye kupewa hilo jukumu. Kwa hivyo, Spika wa Bunge la Kitaifa pamoja na wale ambao wanaratibu jinsi pesa zetu zinatumiwa, waweke fedha katika hii Heroes Act ama Heroes Support Fund ili waweze kupata hiyo"},{"id":1521574,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521574/?format=json","text_counter":134,"type":"scene","speaker_name":"","speaker_title":"","speaker":null,"content":"support"},{"id":1521575,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521575/?format=json","text_counter":135,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Sifuna","speaker_title":"","speaker":{"id":13599,"legal_name":"Sifuna Edwin Watenya","slug":"sifuna-edwin-watenya"},"content":"ambayo watu wanasema wanahitaji kupata. Kwa ajili ya kuenzi huyu shujaa wetu, ni lazima tuangalie hii sheria---"},{"id":1521576,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521576/?format=json","text_counter":136,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kingi","speaker_title":"The Speaker","speaker":null,"content":" Please, give the hon. Senator another thirty seconds."},{"id":1521577,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521577/?format=json","text_counter":137,"type":"speech","speaker_name":"Sen Sifuna","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Bw. Spika, sisi kama Bunge ili tusije hapa tena kulalama jinsi ambavyo mashujaa wengine wanatelekezwa, tuweke fedha katika Bajeti ya mwaka huu kwa sababu tuko katika hiyo cycle ya Bajeti, katika Bunge la Kitaifa na hata hapa. Tuweke pesa kwa ajili ya hii National Heroes Assistance Fund ili tusije kupigwa na butwaa jinsi nilivyomwona Mhe. Wetangula akishtuka. Asante."},{"id":1521578,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521578/?format=json","text_counter":138,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kingi","speaker_title":"The Speaker","speaker":null,"content":" The Senate Majority Leader, please proceed."},{"id":1521579,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521579/?format=json","text_counter":139,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Cheruiyot","speaker_title":"The Senate Majority Leader","speaker":{"id":13165,"legal_name":"Aaron Kipkirui Cheruiyot","slug":"aaron-cheruiyot"},"content":" Bw. Spika, najumuika na Maseneta wenzangu kutoa rambirambi na pia kumshabikia huyu mwanahabari ambaye ni tajika katika taifa letu la Kenya kwa kazi yake aliyoifanya kwa ustadi hadi alipofikia. Kila mwanafunzi wa masomo ya uanahabari, waliokuwa wakati ambapo alikuwa kazini na hata alipostaafu, walikuwa wanatamani wafanye kazi alipofanya. Kwa hivyo, najumuika na wenzangu kutoa pole zetu kama Seneti. Pili, najumuika na Wakenya wote ambao walimshabikia na kusema asante, heko shujaa wetu kwa kazi ambayo umeifanya kwa hali ambayo imewafurahisha Wakenya wote na kusema kweli hapa kulikuwa na mwanahabari. Siyo kila siku ambapo tunapata mtu ambaye baada ya kutuaga, watu wanamshabikia na kusema “Huyo, katika kazi zake, alifanya ilivyotakikana.” Pengine kuna wengine wanajiuliza itakuaje baada ya siku karibu kumi vile tulivyoelezwa na kiongozi, Seneta wa Jiji Kuu la Nairobi, kwamba imekuwa ni siku kumi tangu walipomlaza ndiposa Bunge inazungumzia maswala haya. Ni kwa sababu kazi yake hata baada ya karne kumi bado itakua inakumbukwa katika taifa hili. Jambo la mwisho, nimesikia Maseneta wengi wakitoa mawazo kwamba ingekuwa vizuri kama tungekuwa na Heroes Corner ya kuwashabikia mashujaa wetu. Sisi kama Seneti tunafaa kuwa na kumbukumbu yetu, hata siyo Bunge kwa jumla. Wakenya ama binadamu yeyote ambaye amefanya mambo ambayo sisi kwa kimo chetu kama Seneti tunaona kwamba wamechangia kufika mahali ambapo tunafaa tuwakumbuke. Kwa lugha ya kimombo inaitwa “ hall of fame”. Katika institutions mbalimbali duniani unapata sehemu ambayo wameitenga na kusema kuwa kulingana na sisi tunaona bwana fulani amefanya mambo yake vizuri na inabidi sisi kama chuo au wizara tuwe na kona yetu ya kuwakumbuka watu kama hao. Imefika wakati ambapo ni lazima tuwakumbuke wale ambao wametoa mchango mkubwa kuhakikisha kuwa taifa letu limekuwa bora. Inabidi tuanze na wale waliojitolea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1521580,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521580/?format=json","text_counter":140,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Cheruiyot","speaker_title":"The Senate Majority Leader","speaker":{"id":13165,"legal_name":"Aaron Kipkirui Cheruiyot","slug":"aaron-cheruiyot"},"content":"kuhakiksha kwamba tuna ugatuzi. Tuwaandike na kusema kuwa fulani ni wa kwanza. Hii ni kwa sababu tunajua mchango wake katika kuhakikisha kuwa Kenya kuna ugatuzi. Pengine wale ambao wamezidi katika miaka ya baadaye kuhakikisha kwamba ugatuzi umekita mizizi."},{"id":1521581,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1521581/?format=json","text_counter":141,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kingi","speaker_title":"The Speaker","speaker":null,"content":" Sen. (Dr.) Oburu, you may proceed."}]}