{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=152760","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=152758","results":[{"id":1545782,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545782/?format=json","text_counter":87,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Asante, Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Mwanzo, ningependa kuunga mkono Mswada huu, na vile vile kupongeza Kamati ya Seneti ya Fedha ana Bajeti amabyo inaongozwa na Sen. Roba, kwa kazi nzuri ambayo wamefanya. Jukumu letu kubwa kama Seneti kulingana na Kipengee 96 cha Katiba, ni ugavi wa pesa ambazo zinaenda katika gatuzi zetu na kutetea na kulinda gatuzi zetu. Kiranja wa Wengi, Sen. (Dkt.) Boni Khalwale, amesema ya kwamba sisi ni maadui wa gatuzi. Ningependa kumkosoa kwa sababu sisi sio maadui. Sisi hutetea na kuzilinga gatuzi zetu dhidi ya maadui zake. Bw. Naibu Spika, napongeza vile ambavyo wauguzi wa nyanjani wamepewa hela. Kwa mfano, nikiangalia kwetu, Kaunti ya Laikipia, naona wamepewa Shilingi milioni 25 kwa sababu hao ndio wanafanya kazi nzuri. Ukitembea nchi ya Cuba, utaona hawa wahudumu wa nyanjani ndio wanahusika pakubwa kuwatibu wananchi mashinani. Mgonjwa awe na ugonjwa wa saratani au moyo na magonjwa mengine ambayo yanawaadhiri watu wetu mashinani, ni wao wako kuwaangalia na kuwashughulikia wagonjwa wetu. Bw. Naibu Spika, ni kero katika nchi yetu kupata kuwa hawajalipwa. Ndiposa wakati huu nashukuru kamati kwa sababu tayari wameweka Shilingi milioni 25 ambazo zitaenda kwa wauguzi wetu wa nyajani katika Kaunti ya Laikipia. Ningependa sana kujadili mambo ya Laikipia kwa sababu kila Seneta ambaye yuko hapa anaweza akaguzia kaunti yake. Ukiangalia swala la kulipa madeni ya maafisa wa afya kwenye gatuzi zetu, Kaunti ya Laikipia imetengewa Shilingi milioni 40. Hii itasaidia kwani hivi juzi ulienda kwenye lango la Seneti kuchukua ombi la madaktari hawa. Kila wakati wako kwenye maandamano kwani hawajapewa pesa yao. Tunategemea wauguzi hawa. Ni muhimu kuelewa kuwa unaweza kosa barabara ama elimu lakini ukiwa mgonjwa unaweza ukafa. Ni vizuri sana vile hela hizi zimetengwa ili wauguzi hawa wapate haki yao."},{"id":1545783,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545783/?format=json","text_counter":88,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Ningependa kuangazia CAIPs ambazo zinajengwa ili kuongeza dhamana ya bidhaa zetu. Sijafahamu ujuzi ambao kamati hii ilitumia kuchagua gatuzi ambazo zitapewa hela hizi. Kumbuka kule kwetu Laikipia eneo la Rumuruti, aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda Mhe. Moses Kuria alikuja na kufungua sehemu ile na zaidi ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1545784,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545784/?format=json","text_counter":89,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"ekari 300 zikatengwa kwa sababu ya ujenzi huu. Kulikuwa na sherehe kubwa na mbwembwe. Tulijitolea na kutenga sehemu ile kwa sababu tuna shamba kubwa."},{"id":1545785,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545785/?format=json","text_counter":90,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Serikali kuu iliahidi kutoa shillingi millioni 250 kwa kila gatuzi. Naangalia Mswada huu na naona kuna gatuzi 19 ambazo zimepewa pesa hizi. Sen. (Dr.) Khalwale, amesema tuwe na subira kwa sababu hata kaunti yake haijapewa zile hela, tutaangaliwa kwenye ule Mswada mwingine."},{"id":1545786,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545786/?format=json","text_counter":91,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Swali la muhimu ni hili. Sehemu hizi zimetengwa, tumejua ni bidhaa zipi ambazo tutakuwa tunaongeza dhamana? Tunaweza kujenga, Serikali kuu ilete pesa lakini sehemu hizi zibaki kuwa mahame. Tumeona mambo mengi kama nyumba kujengwa lakini zinabaki kuwa mahame."},{"id":1545787,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545787/?format=json","text_counter":92,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Tukigawa pesa hizi kwenda katika gatuzi zetu, sehemu zile zitumike vizuri. Isiwe tu ni kutengeneza sehemu za kuongeza dhamana kwenye bidhaa zetu na hatuna chochote cha kuongeza dhamana."},{"id":1545788,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545788/?format=json","text_counter":93,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Kaunti ya Laikipia tunakuza nyanya na sisi ni wakulima wa mifugo. Itatubidi tuchague ni kipi ambacho tutaongeza dhamana. Kaunti ya Uasin Gishu wajue ni bidhaa gani wataongeza dhamana ili tusifanye jambo moja sisi wote. Pia kaunti ya Narok inaweza chagua kama ni ng’ombe ama maziwa. Tunashabikia Narok wafanye ile kazi. Kaunti ya Nyamira unapata ni mandizi inaongezwa dhamana. Lakini isiwe ukienda kwenye Kaunti ya Narok, Kisii na Nyamira wote wanaongeza maziwa dhamana. Hii itakuwa ni kazi bure. Lazima tujipange ili tujue ni kaunti ipi itafanya nini."},{"id":1545789,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545789/?format=json","text_counter":94,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Naunga mkono RMLF. Barabara zigawanywa vizuri kama za gatuzi na Serikali kuu. Pia gatuzi zetu zinahitaji zile pesa. Hivi juzi Waziri wa Barabara alikuja na kutuambia kwamba shillingi saba zitatumika kulipa madeni ya Serikali kuu. Lakini hata gatuzi zetu zina madeni. Sisi Wakenya tumetoa shillingi saba kama ushuru wa mafuta tukinunua. Pesa hizi zinafaa kaunti zipate mgao wao. Nikiangalia katika ratiba ya pili, Kaunti ya Laikipia kulingana na ugavi wa fedha hizi za RLMF, tungepewa shillingi millioni 235. Naomba korti zetu ziharakishe kusikiliza kesi hii ili tupate mgao huu. Nitasimama kidete kwa sababu barabara za Laikipi ziko hali mbaya. Bunge la Taifa linaleta mzozo huu ili kaunti zetu zisipate hela hizi. Tutapinga jambo hili leo, kesho, kesho kutwa, mtondo na mtondogoo. Shillingi million 235 zitakazo tengwa kwenda Kaunti ya Laikipia, tusiambie kuwa eti gavana atatumia pesa hizi vibaya. Kuna sheria zitafuatwa. Akitumia pesa vibaya, kuna kamati ambayo inaongozwa na Sen. M. Kajwang’ na nyingine ambayo inaongozwa na Sen. Osotsi ambazo zinaangalia matumizi ya pesa kwa undani katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, tuna wawakilishi wadi ambao hufanya oversight. Pesa zikose kupelekwa katika kaunti kwa sababu ya wizi. Nani alisema Wabunge wa Bunge la Kitaifa ni malaika? Sisi tunapendekeza kwamba pesa hizi zifike katika gatuzi zetu. Katika ratiba ya kwanza kuna makao makuu ya gatuzi zetu ambayo pesa za ujenzi zimetengwa ili makao haya yamalizike. Inasemekana ni makao makuu ya kaunti tano lakini nikiangalia mswada naona ni kaunti nne. Kuna Isiolo, Lamu, Tana River na Tharaka-Nithi. Sijui ya tano ni ipi kwani haiko hapa. Lazima tuwe na marekebisho ili tuongeze pesa ya Nyandarua kwani wanahitaji makao makuu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1545790,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545790/?format=json","text_counter":95,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Bw. Naibu Spika, huwa napitia Ol Kalou nikienda kwetu Laikipia. Naona jumba lile na wasipopewa pesa litakuwa mahame. Ni vizuri hili jambo liangaliwe kikamilifu. Naunga mkono Mswada huu."},{"id":1545791,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545791/?format=json","text_counter":96,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kathuri","speaker_title":"The Deputy Speaker","speaker":{"id":13590,"legal_name":"Murungi Kathuri","slug":"murungi-kathuri"},"content":" Commissioner, Sen. Omogeni, proceed."}]}