{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=152776","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=152774","results":[{"id":1545942,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545942/?format=json","text_counter":45,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Asante, Bw. Naibu Spika, kwa hii fursa umenipa ili kuunga mkono Hoja ya kuidhinisha Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Uhasibu wa Fedha za Umma katika Kaunti. Majukumu ya Seneti imenukuliwa katika Ibara ya 96 ya Katiba ya Kenya. Ibara hii inasema kuwa kazi yetu ni kulinda magatuzi. Katika hekima ya waliotunga Katiba yetu mwaka wa 2010 kuna viwango viwili vya serikali, Serikali za Kaunti na Serikali Kuu. Seneti ikapewa jukumu la kupitisha sheria ya ugavi wa pesa kwa magatuzi. Sheria hii ya ugavi wa pesa kati ya Serikali Kuu na kaunti inaitwa Division of Revenue Act. Pia tulipitisha sheria inayogawanya fedha kwa kaunti 47 inayoitwa County Allocation of Revenue Act. Leo katika hiki kikao maalum tumejadili asubuhi ili kuongeza pesa zaidi ya shillingi billioni 50 kwa gatuzi zetu. Pesa hizi zinaitwa conditional grants. Pesa zikifika kwenye gatuzi wale wanaofanya bajeti ni wafanyikazi wa kaunti kwenye Executive pamoja na Bunge za Magatuzi ama county assemblies. Pia wanajukumu la kutekeleza miradi. Wakati wa kutekeleza miradi kamati za Bunge za kaunti inatakikana kufuatilia miradi hii. Katika uangalizi ama oversight Bunge kwenye kaunti inafaa kufuatilia miradi ifanyike kulingana na sheria, bajeti na uamuzi wa wananchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1545943,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545943/?format=json","text_counter":46,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Mhasibu mkuu anajukumu ya kwenda kwenye kaunti na kuangalia kama pesa zimetumika vizuri. Ibara ya 229 ya Katiba, inaashiria kuwa mhasibu amalize uhasibu wake na kutoa ripoti kufikia Disemba 31 na kuleta ripoti hizi kwenye Bunge. Mhasibu ameleta ripoti zake katika Bunge la Seneti na pia amezipeleka katika mabunge 47 ya gatuzi nchini. Ibara ya 179(4) inakubalia Seneti iitishe ripoti kutoka kwa magavana ambao ni wakurugenzi wakuu ama CEOs kuja katika Kamati na kujibu maswali. Kamati ya Seneti ambayo mimi ni naibu mwenyekiti iliandikia gatuzi zote 47 ambazo ni watendakazi na bunge zao na wakaleta majibu yao. Katika Ibara ya 201 inatakikana kuwa kila gatuzi litumie pesa katika hali ya uwazi. Tukiita magavana walete ripoti za matumizi ya pesa, tunataka kuhakikisha kwamba pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu zimetumika kulingana na sheria. Pia kusaidia yule Mkenya aliye kwenye gatuzi kupata huduma zinazofaa. Vile mwenyekiti wangu ametangulia kusema ni kwamba kuna gatuzi kadhaa ambazo hawakuitika mwito wa kuja mbele ya kamati yetu ya Seneti ili kujibu maswali haya. Kaunti hizi ni Isiolo, Kiambu, Baringo, Marsabit, Nyamira na Kajiado. Gatuzi hizi zilipewa fursa nyingine ili kuja kujibu maswali ya matumizi ya pesa. Ripoti ambazo ziko mbele ya Bunge hii ni tatu. Ripoti ya kwanza ni ya County Executives nay a pili ni ya County Assemblies. Ya tatu ni ripoti ya uaminifu ambayo Bw. Mwenyekiti ameiita Fiduciary Report. Kwa Kiswahili hii ni ripoti ya uaminifu. Tumepitia hizi ripoti zote na kuna masuala kadhaa ambayo imetangulia kujadiliwa tayari ambayo yanaashiria kwamba pesa na mali ya umma katika magatuzi haiko kwenye hali nzuri. Suala la kwanza ni ukosefu wa nakala ya mali na raslimali za gatuzi zetu. Kwa kimombo tunaiita asset register. Wakati nakala ya mali ya gatuzi zetu isipokuwepo, kuna uwezekano wa gatuzi kupoteza mali yao. Kwa mfano, ripoti ya magari mangapi yaliyo katika gatuzi zetu, ripoti ya mashamba yaliyo katika gatuzi zetu. Ni mashamba mangapi hayana hati miliki. Kuna uwezekano wa mashamba haya kupotea kwa sababu hakuna hati miliki kuonyesha kwamba mali hii ni ya kaunti. Jambo lingine ambalo linaashiria kupoteza kwa pesa kulingana na ripoti ya uaminifu ni shida ya kukusanya ushuru wa magatuzi. Gatuzi nyingi zinakusanya ushuru na hazipeleki pesa hizi katika hazina zao. Kaunti nyingi hutumia ushuru baada ya kukusanya ilhali sheria inasema kuwa wakati ushuru umekusanywa upelekwe kwa County Revenue Fund Account. Ushuru utatumika baada ya kufanyiwa bajeti pamoja na pesa zinazotoka kwenye hazina ya kitaifa. Wengine pia wanakusanya ushuru bila kutumia utandawazi. Wakati ushuru unakusanywa bila utandawazi, pesa nyingi hupotea kulingana na ripoti hii ya Mhasibu Mkuu."},{"id":1545944,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545944/?format=json","text_counter":47,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Katika ajira, kaunti nyingi zimeajiri kupita viwango zaidi kinyume na sheria na kanuni zilizowekwa za asilimia 35 ya fedha za kaunti zitumike kulipa wafanyikazi. Mwenyeti amesema ya kwamba kuna kaunti nyingi ambazo zimeajiri wafanyikazi wanaotumia fedha zaidi ya asilimia 35. Wakati tunatumia fedha zaidi ya asilimia 35 kwa mfano katika Kaunti ya Taita Taveta iliyoko katika 54, pesa hubakia kidogo ya kufanya maendeleo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1545945,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545945/?format=json","text_counter":48,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Tunahimiza na kusukuma kaunti kuhakikisha ya kwamba zinafuata kanuni ili fedha zinazotumika kulipa wafanyikazi iwe ni asilimia 35 ama chini yake. Kaunti nyingi zinalipa mishahara za wafanyikazi kupitia nje ya mfumo wa Integrated Personnel and Payroll Database (IPPD) ambao unatumika kulipa wafanyikazi wote wa Serikali. Gatuzi zinapolipa bila kutumia mfumo huu, pesa nyingi sana zinaweza kupotea. Katika kamati yetu, tunafuatilia kwa ukaribu sana ili kuhakikisha kaunti zote zinalipa kupitia kwa IPPD."},{"id":1545946,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545946/?format=json","text_counter":49,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Kuna uchunguzi na mapendekezo mengi tuliyofanya katika hii ripoti lakini tulikuwa na muda mchache sana kama vile Bw. Mwenyekiti alivyosema. Ninashukuru wafanyikazi wa Seneti kwa kujitoa mhanga, kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha ya kwamba hii ripoti ya zaidi kurasa 2,000 imeletwa leo bila kupitisha ule muda uliowekwa katika katika Kifungu cha 229."},{"id":1545947,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545947/?format=json","text_counter":50,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Katika uchunguzi wetu, tumeona ya kwamba kaunti nyingi zinatumia pesa lakini stakabadhi za kuonyesha kwamba zile fedha zimetumika kwa mujibu wa sheria haziko. Kwa mfano, mwanakandarasi amepewa sabuni ya kuleta stakabadhi za kulipwa kama vile invoices lakini amelipwa bila kuwepo kwa zile stakabadhi. Tuko na mapendekezo ya kufuatilia na ndio sababu Bw. Mwenyekiti akasema muda ulikuwa mchache. Kwa hivyo, lazima kuwe na muda zaidi wa kufuatilia ile miradi iliyofanywa katika gatuzi ili kuhakikisha hiyo miradi imefanyika na kwamba wananchi wanapata thamani ya pesa kwa lugha ya kimombo, value for money."},{"id":1545948,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545948/?format=json","text_counter":51,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Tumejiuliza kama kamati itakuwaje mmelipa pesa lakini wakati Mhasibu Mkuu wa pesa ya umma anapokuja kwa kaunti kukagua, hizo nakala zimepotea. Kuna gatuzi nyingi kama vile Bw. Mwenyekiti alivyosema ambazo hazina kamati za ukaguzi ama audit committees. Ukaguzi wa kwanza ni jukumu la kamati za uhasibu za kaunti tunazoziita internal audit. Zinafanya ukaguzi na yule Mhasibu Mkuu anapokuja kukagua, anategemea sana ile ripoti ya kamati ya uhasibu ya kaunti. Lakini kaunti nyingi zimekataa kuwa na hizo kamati kwa sababu kuna mambo wanayoficha huko ndani."},{"id":1545949,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545949/?format=json","text_counter":52,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Sitaki kuongea sana kwa sababu mimi naunga tu mkono hii Hoja. Lakini Mwenyekiti ameongea kuhusu suala la madeni au malimbikizi ya madeni ya kaunti ama pending bills ambazo zimelemaza maendeleo katika kaunti. Yale madeni yanatakikana kulipwa na tukisoma hii ripoti imependekeza ya kwamba taasisi za uchunguzi kama vile DCI na EACC wafanye uchunguzi ili kuona kama yale madeni yalilimbikizwa kihalali. Na kama kuna yale ya kikora, basi hao washukiwa wachukuliwe hatua."},{"id":1545950,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545950/?format=json","text_counter":53,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Kwa sababu Maseneta wanaotaka kuongea ni wengi, sisi kwa ufupi kabisa tunaiomba hii Seneti itupatie fursa tutembelee gatuzi zetu, tuone ile miradi inayosemekana imefanywa, kama imefanywa sawa sawa na kama kuna thamani ya pesa kutokana na pesa ambazo zinatoka kwa ushuru wa mwananchi."},{"id":1545951,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1545951/?format=json","text_counter":54,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mwaruma","speaker_title":"","speaker":{"id":13223,"legal_name":"Johnes Mwashushe Mwaruma","slug":"johnes-mwashushe-mwaruma"},"content":"Serikali haina pesa. Pesa zozote zinazoenda kwa gatuzi zetu zinatokana na ushuru wa mwananchi. Kwa hivyo, sisi wote kama wananchi wa Kenya lazima tufungue macho ili tukiona pesa zinatumika vibaya tuweze kuripoti kwa asasi za uchunguzi. Lazima tuumwe na zile pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu."}]}