{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=153120","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=153118","results":[{"id":1549382,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549382/?format=json","text_counter":98,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"kama mwananchi wa kawaida. Kile alichonacho pengine ni ile sare ya maafisa wa usalama lakini hana chochote kingine. Kwa hivyo, yeye ni kama mwananchi wa kawaida."},{"id":1549383,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549383/?format=json","text_counter":99,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Haya mapendekezo yakipelekwa katika kamati kunapaswa kuletwe mapendekezo yatakayosema hata machifu wanapaswa warejeshewe wale maafisa wao. Kama sio hivyo, machifu wapewe bunduki kwa sababu wanatumika vizuri. Sio tu kwa mambo ya usalama. Hata nakumbuka tulipokuwa wanafunzi tukiwa pale chuoni, kila wakati ukitaka kujaza bursary, chifu angeulizwa kwa sababu anajua kila mwanafunzi na kila mzazi katika sehemu yake. Angeweza kueleza kwa ufasaha ni nani huyu, je kwao ni maskini ili ajulikane vizuri."},{"id":1549384,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549384/?format=json","text_counter":100,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Bw. Spika, naunga mkono Kauli hii ambayo imewasalishwa na Sen. Mwaruma na kukabidiwa Kamati husika. Nawaahidi tutaiunga mkono."},{"id":1549385,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549385/?format=json","text_counter":101,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":{"id":13202,"legal_name":"John Kinyua Nderitu","slug":"john-kinyua-nderitu-2"},"content":"Asante, Bw. Spika."},{"id":1549386,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549386/?format=json","text_counter":102,"type":"speech","speaker_name":"Hon. Kingi","speaker_title":"The Speaker","speaker":null,"content":" Sen. Kavindu Muthama."},{"id":1549387,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549387/?format=json","text_counter":103,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kavindu Muthama","speaker_title":"","speaker":{"id":13733,"legal_name":"Agnes Kavindu Muthama","slug":"agnes-kavindu-muthama"},"content":"Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii nichangie hii kauli iliyoletwa na Sen. Mwaruma. Kauli hii ni muhimu sana kwa sababu manaibu wa machifu na machifu ni watu muhimu sana kwa kila eneo. Utapata ya kwamba hata Serikali ikitaka kujua vile kijiji kinaendelea, wanapitia kwa manaibu wa machifu na machifu."},{"id":1549388,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549388/?format=json","text_counter":104,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kavindu Muthama","speaker_title":"","speaker":{"id":13733,"legal_name":"Agnes Kavindu Muthama","slug":"agnes-kavindu-muthama"},"content":"Naunga mkono kauli hii. Hawa machifu wanapaswa kupewa ulinzi kwa sababu wanafichua njama za watu waovu wanaoweza kuwarudia na kuwaumiza. Hili lina hatarisha maisha yao wanapofichua njama za wahalifu kwenye vijiji."},{"id":1549389,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549389/?format=json","text_counter":105,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kavindu Muthama","speaker_title":"","speaker":{"id":13733,"legal_name":"Agnes Kavindu Muthama","slug":"agnes-kavindu-muthama"},"content":"Pia, ningeomba Sen. Mwaruma na Kamati itakayokabidhiwa Taarifa hii waweze kuangalia hata wazee wa nyumba kumi ambao pia hufanya kazi nyingi sana. Machifu na manaibu wao hawawezi kufanya kazi vizuri bila wazee wa vijiji na viongozi wa nyumba kumi. Wao ndio hufichua kule pombe haramu huuzwa na wahalifu kijijini. Hata mtu aliye mgeni akiingia kwa kijiji, watu wa kwanza kumtambua huwa ni wazee wa kijiji, chifu na naibu wao."},{"id":1549390,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549390/?format=json","text_counter":106,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kavindu Muthama","speaker_title":"","speaker":{"id":13733,"legal_name":"Agnes Kavindu Muthama","slug":"agnes-kavindu-muthama"},"content":"Ni vizuiri pia wawe wanapandishwa vyeo kulingana na muda uliowekwa. Pia, Kamati inapoenda kuangalia Kauli hili, wahakikishe pia hawa wazee wanalipwa. Wazee hawa huamshwa usiku wa manane kwenda mahali kuna mgonjwa au uhalifu bila kuogopa ilhali hawapewi chochote na Serikali. Kwa hivyo, ni vizuri hata hao wazee wa nyumba kumi wawe wanalipwa ama wapewe pesa ya usafiri ili kwenda kule wanakohitajika."},{"id":1549391,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1549391/?format=json","text_counter":107,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kavindu Muthama","speaker_title":"","speaker":{"id":13733,"legal_name":"Agnes Kavindu Muthama","slug":"agnes-kavindu-muthama"},"content":"Utapata hata polisi kufanya kazi nzuri katika stesheni zao inabidi watumie machifu na manaibu wao na wazee wa nyumba kumi ili wapate ripoti za wale wahalifu mahali waliko."}]}