{"count":1608389,"next":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=160730","previous":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/?format=json&page=160728","results":[{"id":1625482,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625482/?format=json","text_counter":233,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"The Senate Minority Leader","speaker":null,"content":"Bi. Spika wa Muda, hakuna sheria za Kenya zinazompa Waziri ama Mhe. Rais ruhusa ya kuagiza Mkenya apigwe risasi. Ni jambo la kusikitisha. Matamshi kama hayo yanatakikana kuzuiliwa kwa kuwa hayaungwi mkono na Katiba. Ni kinyume cha sheria."},{"id":1625483,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625483/?format=json","text_counter":234,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Madzayo","speaker_title":"The Senate Minority Leader","speaker":null,"content":"Ukitoa amri ya kwamba ----"},{"id":1625484,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625484/?format=json","text_counter":235,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Ninaunga mkono Taarifa iliyoletwa na Sen. (Dr.) Khalwale kuhusu maandamano."},{"id":1625485,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625485/?format=json","text_counter":236,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ibara ya 37 ya Katiba ya Kenya inakubali maandamano ya amani. Inavunja moyo sana ukiona watu wanaandamana wengine kwa amani ilhali kuna wahuni. Jambo la kuvunja moyo zaidi ukitembea Nanyuki – kwa sababu kulikuwa na maandamano ya Saba Saba - msichana wa miaka 24 ambaye ni Julia Njoki alishikwa, akapelekwa kortini na kuhukumiwa. Kwa njia isiyojulikana alifia katika seli."},{"id":1625486,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625486/?format=json","text_counter":237,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Amri inasema Wakenya wapigwe risasi lakini Katiba ya Kenya inasema kazi ya Serikali kuu ni kulinda mali na maisha ya wananchi."},{"id":1625487,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625487/?format=json","text_counter":238,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Ikiwa kuna wahuni wanaoingilia maandamano na kuleta vurugu, kuiba, kudhulumu na kuumiza wananchi, kuna mpangilio unaofaa kufuatwa wa kushikwa, wapelekwe kortini na kuhukumiwa kwa sababu sheria zetu zinasema mtu hana hatia mpaka ithibitishwe kortini."},{"id":1625488,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625488/?format=json","text_counter":239,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Sio Julia Njoki pekee. Kijana wa kidato cha tatu, James Gachara, alipigwa risasi na kuuawa wakati wa kuadhimishwa kwa siku ya Saba Saba. Je, alikuwa amebeba nini?"},{"id":1625489,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625489/?format=json","text_counter":240,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Kuna haya mambo ya kushambulia watu wakiwa katika maandamano ilhali wahuni wanaendelea kufanya kazi yao bila kusimamishwa na askari yeyote. Jana niliangalia nikaona ya kwamba nyanyake Julia Njoki ni mama mkongwe. Hata yeye alipigwa na hewa ya kutoa machozi akitetea haki ya mjukuu wake. Babake msichana huyo, Martin Kariuki Rienye, ndiye chifu wa sehemu hiyo. Hata mfanyikazi wa Serikali anavunjwa moyo na hawa askari wanaopenda kupiga watu risasi."},{"id":1625490,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625490/?format=json","text_counter":241,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Kinyua","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Bi. Spika wa Muda, hili ni jambo lisilopaswa kukubalika katika nchi yetu. Kamati ya Usalama inapaswa kuangalia mambo hayo kwa undani ili wajue wahuni ni akina nani- -- The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."},{"id":1625491,"url":"http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625491/?format=json","text_counter":242,"type":"speech","speaker_name":"Sen. Mungatana, MGH","speaker_title":"","speaker":null,"content":"Thank you, Madam Temporary Speaker for giving me the opportunity to take the Floor and support the Statement by Sen. (Prof.) Kamar on labour migration and the consultations that were made by Pan African Parliament (PAP) here in Nairobi on 16th June, 2025."}]}