John Kinyua Nderitu

Parties & Coalitions

All parliamentary appearances

Entries 1 to 10 of 1910.

  • 28 Sep 2023 in Senate: Mr. Speaker, Sir, I have listened to Sen. Wafula and he has asked whether he can commit to the Standing Committee on Labour and Social Welfare, but that matter is not within Kenya. I thought it was supposed to be committed to the Standing Committee on National Security and Foreign Relations. Just a point of clarification. view
  • 28 Sep 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Ni jambo la kuvunja moyo sana kwamba wakenya wametoka nchini kutafuta ajira kwenye nchi za ng’ambo na wanakumbwa na mashaka. Hata hivyo, Serikali ya Kenya Kwanza tayari inajaribu kuangazia mambo haya. Kwa mfano, Serikali tayari imeajiri wauguzi wa nyanjani zaidi ya 100,000. Vile vile, Serikali imepeana pembejeo ndiposa wakulima wetu wapate afueni. Kamati itakayoangazia swala hili, yafaa iiangazie kwa undani ili tupate suluhu la kudumu. Shule zetu zinapaswa kuwalinda Watoto wanaposafiri. Seneta wa Nyeri, amesoma Kauli na kuashiria kuwa kuna wanafunzi waliosafiri na kupata shida na hatimaye mmoja wao akafa. Walimu wanaposafiri na ... view
  • 28 Sep 2023 in Senate: On a point of Order, Madam Temporary Chairperson. view
  • 28 Sep 2023 in Senate: Madam Temporary Chairperson, the Senator of Nairobi City County has just come in with some weapon. view
  • 28 Sep 2023 in Senate: No, it is important. This is a House of Order. view
  • 21 Sep 2023 in Senate: Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Ninaunga mkono Taarifa ya Sen. Okenyuri. Mambo ambayo yanatokea katika sehemu za kujiburidisha yamekuwa donda sugu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 21 Sep 2023 in Senate: Ukitembelea sehemu nyingi, unapata watu ambao wanajifanya wameenda kuburidika lakini wanavizia wengine; ni wakora. Wamebeba dawa ambayo inajulikana kwa Kingereza kama Dormicum. Wanawekea watu wakati wameenda kujiburudisha na hawana nia yoyote. Unapata mtu amewekewa dawa ambayo, kwa lugha ya mtaani inaitwa ‘mchele’ na baada ya dakika chache, wanalala na kukosa fahamu, na kuibiwa. Wengine wanakubeba na kukupeleka kwa gari na kukuibia chochote ulichonacho. Kwa hivyo, Kamati ya Usalama inaposhughulikia jambo hili, waliangalie kwa undani duka za kuuza madawa kwa sababu hapo ndipo shida huanzia. Kuna madawa ambayo imekubalika kuuzwa lakini inapaswa kuuzwa kwa mtu aliye na prescription . Unapata watu ... view
  • 31 Aug 2023 in Senate: Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada huu wa mabadiliko ya tabia nchi ama hali ya hewa. Bw. Spika, ni vizuri kulinda mazingira. Upanzi wa miti ni wa busara sana katika nchi. Kile ambacho kimekuwa kinavunja moyo ni kwamba mtaala wetu wa masomo hauzingatii zaidi mambo ya mazingira na ukulima. Nakumbuka tukiwa wanafunzi tulikuwa tunazuia mmonyoko wa udongo. Lakini, kila wakati tukipewa motisha tuliambiwa tusome tuwe madaktari, wahandisi na marubani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate. view
  • 31 Aug 2023 in Senate: Mkulima na wanaojihusisha na mambo ya upanzi wa miti na utunzaji wa mazingira, hawakuchukuliwa kuwa muhimu. Ndiposa wakati huu, nchi ambazo zimeendelea ndizo zinajua ni pesa ngapi watatoa ridhaa kwa kaboni. Hata sisi, sheria tunayoipitisha itasaidia sana. Ukitembea Laikipia, kuna Misitu kama vile, Rumuruti, Lariak na Mukogodo. Lakini, watu walio huko hawafaidiki na misitu waliyonayo. Ukitembea Kaunti ya Kilifi, anakotoka Kiongozi wa Waliowachache, Sen. Madzayo, tuliwaona wananchi wa zile sehemu wakisema hawaoni faida yeyote ya ile mibuyu. Tayari wanaing’oa na kuiuza katika nchi za ughaibuni. Hawaoni faida yeyote. Kwa hivyo, Mswada huu ukipita, tungetaka kujua wale ambao wanakuja kutupatia ridhaa ... view
  • 31 Aug 2023 in Senate: Bw. Naibu Spika, tumeketi na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu. Ni desturi yetu wanafunzi wanapokuja hapa, ili kuwapa motisha, tunawataja kwa majina. Najua shughuli ya leo ni ya dharura, lakini ni vizuri kuwataja kwa majina ndiposa tuwape motisha. Bw. Naibu Spika, naskia watu wengi wakisema mambo ni magumu. Lakini, tuwape motisha viongozi wa kesho. view

Comments

(For newest comments first please choose 'Newest' from the 'Discussion' tab below.)
comments powered by Disqus