GET /api/v0.1/hansard/entries/542991/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 542991,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/542991/?format=api",
"text_counter": 50,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Asante sana. Mimi pia nataka kuchukua fursa hii kumushukuru dada yangu Mheshimiwa Joyce Lay kwa ajili ya Hoja hii. Tunapotafsiri Katiba yetu katika lugha ya Kiswahili itatupa nafasi nzuri ya kuelimisha watu wetu, hasa kuhusu mambo ya ndoa na jinsia katika nchi yetu ya Kenya. Vile wenzangu wamesema, hata mkiwaona vijana wetu wanaoendesha pikipiki ama bodaboda unajua hawaelewi Katiba yetu. Itakuwa ni vyema kuona kwamba Katiba yetu imetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili na hiyo itatupa nafasi nzuri sana. Ninamshukuru dada yangu, Mheshimiwa Joyce Lay kwa kuleta Hoja kama hii katika Bunge. Ahsante sana."
}