GET /api/v0.1/hansard/entries/584611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 584611,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/584611/?format=api",
    "text_counter": 230,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi kuchangia Hoja hii. Kwanza, natoa shukrani za dhati kwa Sen. Mutula Kilonzo Jnr. Nafikiri kwamba katika maono yake, ameona kwamba sio jambo la eneo fulani bali ni Wakenya wote walioko katika janga hili la dhuluma ya mashamba. Nampongeza kwa kuleta Hoja hii. Maonevu na wizi wa mashamba ni kama ugonjwa wa saratani ambao ni ngumu kupona na lazima mtu apewe matibabu mengi sana. Sisi tuko katika historia sasa na hivyo ningependa kusema kwamba watu wanoitwa maskwota, walala hoi au maskini ambao hawajiwezi wameteswa na mabwenyenye. Hilo ni jambo la kusikitisha kwa sababu nikitoa mfano wa Kaunti ya Kilifi, karibu kaunti yote, watu ni maskwota na ni jambo la aibu sana kwamba tangu Uhuru upatikane Kenya, watu ambao wana hati miliki za ardhi ni wachache sana. Ni maonevu ambayo ni dhambi kubwa sana hata mbele ya Mungu. Kilio cha wanyonge cha watu wa Pwani ni The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}