GET /api/v0.1/hansard/entries/585497/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 585497,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/585497/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ngunjiri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1179,
        "legal_name": "Onesmas Kimani Ngunjiri",
        "slug": "onesmas-kimani-ngunjiri"
    },
    "content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninashukuru. Yangu yatakuwa machache kwa sababu mimi ni mwanachama wa Kamati ya Ardhi. Ningependa kumshukuru Mwenyekiti wangu kwa kazi nzuri ambayo amefanya kwa Kamati yetu. Kamati ya Ardhi inafanya mambo yote ambayo inaweza kufanya kuhakikisha kwamba mjadala kama huu kuhusu shamba la Muri umetimia na mambo haya yamemalizikika. Lakini, ningetaka kuweka wazi ili kila mtu aelewe na Serikali ielewe kuwa baada ya Kamati ya Ardhi kumaliza mambo haya yote, shida nyingi zinatokea baada ya sisi kutoa maoni yetu. Shida hutokea baada ya kuanza kuwapatia cheti cha mashamba yao. Hapo ndio watu huingilia na kuuharibu mpangilio ambao umepangwa na Serikali. Ningewaomba wale ambao watahusika baada ya Bunge kutoa muongozo wake, waangalie kwa makini sana ili tusirudi kwa shida baada ya kusema kuwa tunataka kuyamaliza mambo haya. Wale ambao hawana mashamba wanafaa kupata mahali pa kukaa. Ukiangalia shamba hili ambalo tunazungumzia, utakuta kuwa vitukuu vinaendelea kuwa na vizazi na maskwota wanaendelea kuongezeka usiku na mchana. Tukitatua jambo hili haraka iwezekanavyo, tutapunguza umaskini. Hawa watu wakipata vyeti vya kumilika mashamba, watasaidika kwa njia zingine kama vile kujaribu kupata mashamba mengine madogo kwa familia. Ni lazima tujue kuwa kuna shida. Tukimaliza mambo ya mipangilio, ni lazima tuhakikishe kuwa wale ambao wanahusika kama vile Tume ya Ardhi au Wizara ya Ardhi inafanya mambo haya kwa uwazi. Wakati tulikuwa na shida ya IDPs, watu wengi ambao walipewa makao sio wale ambao walikuwa IDPs. Baada ya Serikali kutoa shamba ya kuwapa IDPs, mambo mengi yalitokea badaye. Ningetaka kuambia maofisa wa Serikali, wanapowapatia watu mashamba, wanafaa kuangalia kwa makini sana ili wasilete orodha zingine ambazo si za watu ambao wanafaa kupewa hayo mashamba. Hiyo italeta shida juu ya shida. Kwa hivyo, Kamati yetu inafanya iwezavyo chini ya uongozi wa Mwenyekiti wetu, Mhe. Mwiru, ambaye anafanya kazi nzuri. Ninashukuru kusikia Wabunge wanaunga mkono jambo hili. Wanaiunga mkono Kamati ya Ardhi kwa kazi ambayo tunayoifanya. Tuko na mengi ambayo tumetayarisha kuleta Bungeni. Tukiwachia Wizara ya Ardhi na Tume ya Ardhi jambo la kufuatilia utaratibu wa mipangilio ya mashamba, tungetaka waifuatilie ili isilete aibu tena au isisemekane kuwa wale ambao tulipendekeza wapewe mashamba sio wao walipewa na watu wengine walipewa. Jambo hili linaleta shida sana. Ninamshukuru Mwenyekiti wetu kwa kazi nzuri. Ninamshukuru Mbunge wa eneo hilo kwa sababu alitupeleka kwa shamba hili na tukaona vile liko. Ningetaka mambo haya yafuatiliwe bila kupita njia nyingine kwa sababu Kamati ya Ardhi katika Bunge iko na haki ya kuyamaliza mambo haya ambayo yaliletwa Bungeni. Kwa hivyo, ninashukuru Bunge kwa kutuunga mkono. Tuendelee hivyo hivyo na tutapata nguvu."
}