GET /api/v0.1/hansard/entries/586917/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 586917,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/586917/?format=api",
    "text_counter": 324,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, sitaki kusema kwamba uzee umemuingia mwenzangu. Nilisema kuhusu hata Wakuria, Wakisii na makabila mengine yote 42. Hata Mmasaai anaweza kufanya vizuri katika mbio za nyika. Kuna michezo mingi ambayo inastahili kuungwa mkono. Kuna Mkenya mmoja ambaye amefanya vizuri katika mchezo wa kurusha mkuki licha ya kuwa alijifunza mchezo huo mwenyewe kupitia mtandao. Hivi sasa tunampigia makofi na vigelegele. Kuna mchezo mwingine wa kurusha mishale kupitia upinde. Mmeru au Mkuria akipewa nafasi hiyo anaweza kufanya vizuri. Hata hivyo, wengi wao hawajui kwamba kuna mchezo kama huo. Pia, kuna mchezo wa kutupa sahani na jiwe kuu. Hii ni michezo ambayo Wakenya wengi wanaweza kufanya vizuri. Nina uhakika kwamba Sen. Karaba akipata nafasi hiyo anaweza kuitupa mbali sana. Lakini wengi wetu tunafikiri kwamba michezo inahusu tu riadha. Baada ya wanariadha wetu kufanya vizuri kule ng’ambo, wanaporudi nchini wanapokelewa na Waziri siku zingine. Lakini wakati mwingi wanarudi na kupokelewa na jamii zao tu. Hata magazeti huripoti habari hizo katika kurasa zao za mwisho. Hii ni licha ya kwamba wanariadha wetu wanatuletea rasilmali kubwa hasa pesa za kigeni wakati utalii na kilimo cha kahawa na chai kimeathirika. Shukurani yetu ni mateke ya punda. Nawasifu na kuwashukuru wengi wa wanariadha wanaorudi nchini na kuekeza pesa zao vizuri. Wengi wamejenga nyumba, hoteli nzuri na maduka makubwa. Je, kama sisi ni wazalendo, tumewafanyia nini? Tukiwatambua, kuwatuza medali wanazostahili vile Sen. Melly alisema, huenda tukawatia moyo wengine ambao wana vipawa ili wafanye vizuri. Wengi wao wanapatikana katika shule, lakini pia kuna wale hawakuenda shule na wanaweza kukimbia. Mtu hahitaji kuwa na elimu ya kemia au kufika Darasa la Nane au Kidato cha Nne ili atambulike kwamba anaweza kukimbia. Kwa hivyo, tunafaa kuunda sera na desturi mashinani za kuwatambua hata wale wanariadha ambao hawakuenda shule. Kuna wanariadha wengi kama hao kule vijijini. Hawana namna ya kutambulika kwa sababu hawakupata nafasi ya kwenda shule. Viwanja vinafaa kujengwa katika vijiji ili watu wote wenye vipaji wapate nafasi. Hatua hii itawapa nafasi wanariadha wote hata wale hawakuenda shule na wale wanaojificha kule mashinani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}