GET /api/v0.1/hansard/entries/610495/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 610495,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/610495/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Shukrani sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Hoja hii ambayo imeletwa na Mheshimiwa mwenzetu. Ninampongeza mheshimiwa kwa kuwa hii ni Hoja muhimu kwa maisha ya Mkenya. Ningependa kumpongeza kwa kuwa ametambua kwamba ni wachache wametambulika katika kufidiwa na wakoloni. Kwa kweli, upiganiaji wa Uhuru haukuwa katika sehemu moja ya Kenya hii; ulikuwa katika kila pembe za nchi hii. Kwa sababu ya hali ya umaskini uliowakabidhi watu wetu katika maeneo mengine, mpaka sasa, hawajaweza kwenda kortini ili kutetea haki zao. Ni wajibu wa Serikali kusimama kidete kuwatetea Wakenya. Ninamshukuru mheshimiwa kwa kuwa ameweza kuyataja maeneo husika lakini kwa uchache, ningependa pia kuwataja mashujaa kutoka sehemu ya Kwale maana kunao walioweza kujitokeza na kupigania uhuru wa nchi hii; kwa mfano, Mzee Bilashaka, Mzee Mwamgunga, Mzee Mbembe, Mzee Bambaulo na nyanya yangu, ambaye alikuwa mpishi wa wapiganaji wa Mau Mau . Mababu zangu pia walikuwa wapishi wa wapiganaji wa"
}