GET /api/v0.1/hansard/entries/632247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 632247,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/632247/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Bunge linapopitisha masuala kama haya, linatatua matatizo ambayo yapo. Matatizo haya yapo na hayajatatuliwa hususan tukizungumzia Pwani. Mbali na hayo, walikuwa na imani kubwa katika Tume ya Kitaifa ya Ardhi. Mpaka wakati huu, Tume hii bado haijatatua matatizo kwa kisingizio kuwa Wizara ya Ardhi haijawapa mamlaka kamili au inawanyima haki yao ya kufanya kazi. Ikiwa kisingizio hicho kitaendelea kwa namna hii, ina maana kuwa yale malengo ya Wakenya kuipigia Katiba kura yatakuwa hayajapatikana. Tukizingatia muda ambao umepita tangu Wakenya waipigie Katiba kura mpaka leo ambapo Mswada huu umefika Bungeni ili tujadili jinsi tutawasaidia Wakenya kama viongozi na wawakilishi wa kila sehemu, tunahitaji kuhakikisha kuwa Mswada huu utakapopita hapa Bungeni, utapita na mwongozo na matakwa ya kisawasawa ili kutitimiza ndoto za Wakenya. Ningependa kukoma kwa kusisitiza kwamba ni muhimu Mswada huu ushambuliwe na ikiwezekana ugawanywe katika sehemu tatu ili ujadiliwe kikamilifu. Namna ulivyochanganywa, nina imani kuu kwamba itawafanya wengi wasifahamu kinachoendelea. Hii itasababisha Mswada huu kupitishwa ilhali tunarejesha ile ile Kenya ya zamani ambapo mtu wa kawaida hapati haki yake."
}