GET /api/v0.1/hansard/entries/638062/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 638062,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/638062/?format=api",
    "text_counter": 559,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda. Nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii haswa ukijua kwamba nilikuwa kapteni wako kule Malindi. Ninaiunga mkono Hoja hii kwa sababu kuna haja kubwa ya walemavu kushughulikiwa kikamilifu na Serikali yetu. Walemavu wamekuwa wakihangaika sana. Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba majengo yamefanyiwa ukarabati na kupigwa msasa. Ngazi katika majengo yote zinapaswa kufanyiwa marekebisho ili kuwawezesha walemavu kuzitumia. Kuna haja magari, kuanzia sasa, yatengenezwe ikijulikana kwamba kuna watu ambao hawawezi kuinua miguu yao na kuabiri. Magari yanapaswa kuundwa kwa namna ambayo itawawezesha walemavu kuabiri bila ya kupata usaidizi kutoka kwa mtu yeyote."
}