GET /api/v0.1/hansard/entries/639960/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 639960,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/639960/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante Mhe. Naibu Spika kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii. Kwanza, ningetaka kumpongeza Mhe. Wanga kwa wazo lake zuri la kuweza kuokoa maisha ya Wakenya wengi. Kwa hakika, moyoni ninaona kwamba mtu mmoja katika kila kaunti ni idadi ndogo. Lakini kulingana na maelezo ya Mhe. Wanga, si neno maanake ni chanzo. Safari ndefu huanza na hatua ya kwanza. Hivyo basi, ningeuliza pia wenzangu waweze kuunga mkono Hoja hii ili tuweze kubuni vituo katika kila kaunti ambavyo vitakuwa vikifanya uchunguzi wa mapema ili kung’amua saratani aina mbalimbali na itibiwe mapema. Ni dhahiri kwamba sote katika Bunge hili tunaelekea huko kwa sababu chanzo cha saratani huwa ni vigezo tofauti hasa wale ambao hupenda kutumia chai moto sana. Chai moto sana inapotumika kwa muda mrefu husababisha saratani ya koo. Hivyo basi, ni muhimu sana kwamba vituo hivi vibuniwe katika kila kaunti. Vilevile, wakati umefika wa nchi hii kujitegemea kwa wataalam. Mara kwa mara, tunatuma wagonjwa wetu nchi za ng’ambo ili kuenda kuhudumiwa na wataalam. Wakati ni sasa wa kuwa na wataalam wetu wenyewe na mtaalamu mmoja kwa kila kaunti kila mwaka sioni kwamba itakuwa sehemu kubwa katika makadirio ya mwaka katika Serikali."
}