GET /api/v0.1/hansard/entries/640022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 640022,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640022/?format=api",
    "text_counter": 163,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bedzimba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1933,
        "legal_name": "Rashid Juma Bedzimba",
        "slug": "rashid-juma-bedzimba"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa ili pia nipenyeze sauti yangu kwenye Hoja hii. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii. Karibuni, kulikuwa na matokeo yaliyoonyesha kuwa Wakenya wengi wanatumia pesa nyingi kwa matibabu ya saratani ng’ambo. Ni vyema Serikali itilie maanani jambo hili ili iweze kujenga sehemu ambazo saratani itatibiwa katika sehemu zote za ugatuzi. Hata tukiwaelimisha watu kwamba wapimwe mapema wajue kama wana saratani ili watibiwe, wengi wanaogopa kupimwa kwa sababu wana hakika kwamba hakuna pahali watapata matibabu. Ni vyema Serikali itenge fedha na ihakikishe kwamba kila eneo la ugatuzi lina vifaa maalum vya saratani ili watu wapimwe pale na waanze matibabu pale. Ikiwa litakuwa jambo nzito, ndipo wanaweza kwenda kwa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta. La muhimu ni kwamba kila sehemu ya ugatuzi yafaa ijitegemee kwa matibabu ya saratani. Ugonjwa wa saratani umepoteza maisha ya watu wengi sana. Imekuwa sasa kama jambo la kawaida. Mtu anafikiria anapopatikana na ugonjwa wa saratani, tayari amepata tikiti ya kuelekea ahera. Ni vyema Serikali itilie mkazo jambo hili. Namshukuru Mhe. Wanga kwa kuleta Hoja hii. Hajaileta hapa Bungeni ichangiwe tu. Hatakosa kitu kutoka kwa Mungu kwa sababu saratani imewadhuru wanannchi wengi, haswa katika mashinani."
}