GET /api/v0.1/hansard/entries/640032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 640032,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640032/?format=api",
"text_counter": 173,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ahsante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi kuunga mkono Hoja hii. Wenzangu wamezungumzia ugonjwa huu na kwa kweli, umeathiri watu wengi. Tunaomba Serikali iangalie njia zinazoweza kutumika kuzuia ugonjwa huo. Watu wengi nchini Kenya hawaelewi chanzo cha ugonjwa huo. Watu wengi wamekufa. Wakati watu wanaenda kutafuta matibabu, wanaambiwa kuwa hakuna njia ya kutibiwa kwa sababu ugonjwa umeenea sana. Kwa sasa, HIV/AIDS ni afadhali kwa sababu kumepatikana madawa ya kusaidia watu kwa muda mrefu. Ingefaa tuwe na njia ya kupima watu mapema ili waanze kutibiwa. Tumeleta watu wetu wengi Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta lakini mara nyingi, madaktari wanasema kuwa hakuna njia ya kutibiwa kwa sababu saratani imeenea sana mwilini. Madaktari wanafaa wapime watu mapema kabla saratani haijaenea sana mwilini."
}