GET /api/v0.1/hansard/entries/640040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 640040,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640040/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Aburi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2901,
"legal_name": "Lawrence Mpuru Aburi",
"slug": "lawrence-mpuru-aburi"
},
"content": "Kama inawezekana, tuwe na madaktari kule mashinani wa kuwashughulikia watu hao. Nikimalizia, nawaeleza Wakenya ambao wanatusikiliza tukiongea kwamba pesa ambazo zinapelekwa kwa serikari za kaunti zinapitia katika Bunge hili kama Bajeti. Kwa mfano, tunajua pesa za Kajiado, Kilifi, Mombasa, Nairobi, Kericho na Meru ni ngapi. Hizo pesa ni nyingi na zimepewa kaunti ili washughulikie hospitali lakini zikifika huko, hazishughulikii mwananchi wa kawaida aliye na taabu nyingi sana. Ukienda Hospitali ya Meru, haiko vile ilivyokuwa wakati wa Rais mstaafu Kibaki au “Nyayo”. Ilikuwa safi sana na haikuwa na harufu yoyote. Hivi sasa, watu wanaoishi karibu na chumba cha kuhifadhia maiti cha Meru wameanza kuhama. Pesa hizo ambazo Serikali kuu inapatia serikali za kauti ili zishughulikie hospitali za kaunti huenda kwa hospitali za kibinafisi, au kwenye mifuko yao. Naunga mkono Hoja hii ya Bi. Wanga. Itawezesha kuwa na madaktari kule mashinani."
}