GET /api/v0.1/hansard/entries/640104/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 640104,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640104/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Mambo ya saratani ni mambo ambayo yamesumbua wananchi wengi wa Kenya. Ninavyozungumza, mimi binafsi katika ofisi yangu pale mashinani, nina mmoja wa wafanyikazi wangu anayeugua saratani ya matiti. Ilituchukuwa karibu miaka miwili kumfanyia Harambee mpaka akatolewa lile titi na akawekwa lile titi bandia. Jambo hili ni la kusikitisha kwa sababu yeye aliwapata watu wa kumfanyia Harambee lakini wengine wasio na uwezo wa kufanyiwa mambo kama hayo, inakua ni shida. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunaona athari ya ugonjwa wa saratani kwa watu wengi katika sehemu nyingi nchini. Watu wakitaka kupata matibabu, mpaka waje kwa Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, Nairobi. Kwa Serikali yetu ya Kenya, tunasema kuwe na vifaa vya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}