GET /api/v0.1/hansard/entries/640105/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 640105,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/640105/?format=api",
"text_counter": 246,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "kuangalia mambo ya ugonjwa wa saratani na viwekwe katika kila sehemu na nyanja ya nchi yetu ya Kenya. Mhe. Naibu Spika wa Muda, zaidi, tunaona ugonjwa wa saratani unasababishwa na mambo ya vyakula. Kupitia kwa wizara inayohusika na mambo ya afya, ni vizuri kuona kuwa vyakula vinavyoingia nchini vimethibitishwa kuwa sawa. Isiwe vyakula vinavyowachiliwa kuingia nchini na kusababisha magonjwa kwa wananchi wetu. Tukiangalia hali ya kutibu magonjwa ya saratani, imekuwa hali ngumu kwa sababu wagonjwa waathiriwa wanapokuja Nairobi, inabidi watafute pesa za kutibiwa kwa kila hatua ya matibabu. Wengi wao hufuata viongozi kama sisi na kuwaambia wanatakiwa kufanyiwa matibabu hospitali fulani kwa wakati fulani. Hivyo, wao hutaka pesa za matibabu na makaazi katika sehemu ya hospitali. Naomba Serikali iwe na hazina. Kwanza, ingetangaza mambo ya saratani kuwa janga la kitaifa kama ilivyotangaza Ukimwi. Vile vile, Serikali iweke pesa fulani zitakazosaidia kiwango fulani cha waathiriwa wa saratani kujikimu. Hii ni kwa sababu wengi wameharibu maisha yao kwa kugharamia matibabu. Watu wanafanya kazi ili wasomeshe watoto, waweze kujikimu maishani na kwa mambo mengine mbali mbali. Lakini utamuona mtu anafanya kazi na pesa zote zinaenda kwa matibabu kwa miaka mitano, 10 ama 20. Kwa hivyo, twatakikana twende mbele. Kwa sababu ya ugonjwa wa saratani, maisha ya binadamu ni kama wasemavyo Waswahili: “kiribagoji–gojikiriba.” Yaani, huendi mbele. Mtu huwa yuazungukia hapo hapo. Naiomba Serikali itilie maanani mambo haya ya kutibu saratani. Sisi kule mashinani katika hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge, ni vizuri kuwe na kiwango fulani cha kusaidia kwa matibabu kama hayo. Mwisho, nataka kumpongeza dadangu Mhe. Gladys kwa kuja na jambo kama hili. Tutamuunga mkono kama Wabunge kuona kuwa tumepitisha Hoja hii kwa njia ya sawa ili wananchi wetu wawe sawa. Ahsante sana kwa kunipa nafasi, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}