GET /api/v0.1/hansard/entries/674999/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 674999,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/674999/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Shukrani Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi na heshima niliopatiwa na Mheshimiwa Malulu Injendi. Naunga mkono hii Hoja ambayo ni muhimu sana. Mimi mwenyewe nilikuwa nimeandika Hoja kama hii lakini ikawa mwenza amenitangulia. Sina budi bali kumuunga mkono kwa kila namna. Mheshimiwa Naibu wa Spika wa Muda, mwanzo kabla hata sijaongea sana, hao wazee wa kijiji sio lazima wawe na elimu kiwango fulani bali lazima wawe ni watu tu ambao wamechaguliwa na wananchi kule vijijini. Hao wazee wa vijiji wakiwa wazee kwa wamama hufanya kazi kubwa haswa kwa masuala ya usalama ambalo ni jukumu muhimu sana kwa nchi yetu kwa ujumla. Maanake inachangia kwa masuala ya uchumi kama vile utalii, uchumi na kile kitengo kwa ujumla maanake hata ukila Ugali na hakuna usalama, huo Ugali hausimami tumboni. Mhe. Naibu Spika wa Muda, hawa wazee wa vijiji huchangia sana. Wao hufanya kazi kubwa. Saa zingine wanaamka masaa ya usiku sana na hawana tochi, viatu, nguo na hawalipwi, na ilhali wanachangia pakubwa sana katika shughuli tofauti za nchi yetu kuleta maendeleo kule mashinani. Miaka ya nyuma, wazee wa vijiji walikuwa ni watu ambao wamekomaa, wamefundisha watoto wao wakamaliza, na wengine wamepumzika kule mashinani, lakini hali imebadilika. Siku hizi wazee wa vijiji ni vijana ambao wameoa juzi, na akina mama pia wako na watoto wanasoma. Nampongeza sana Mhe. Injendi kwa kuleta Hoja hii."
}