GET /api/v0.1/hansard/entries/675010/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 675010,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675010/?format=api",
    "text_counter": 121,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Chea",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1694,
        "legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
        "slug": "mwinga-gunga-chea"
    },
    "content": "Ukiangalia katika Katiba yetu, suala la usalama limeachwa katika Serikali ya Kitaifa. Serikali za kaunti zinahusika kwa kiwango fulani katika suala hili, lakini Serikali ya kitaifa ndiyo imewekewa jukumu hili la usalama. Baadhi ya wale washikandao katika suala hili la usalama ni wazee wetu wa vijiji. Waheshimiwa wenzangu wataniunga mkono kwamba kila mara tunapoenda kwa mikutano kule nyanjani, masuala mengi huzungumzwa lakini suala ambalo utaulizwa kama kiongozi wa kitaifa ni ajira kwa wazee wa vijiji. Mhe. Injenda ameeleza dhahiri shahiri kwamba katika ngazi ya Serikali ya kitaifa, kuna makamishna ambao wanategemea zaidi habari na ushauri kutoka kwa wazee wetu wa vijiji. Kinachoshangaza ni kwamba ukiangalia tofauti ya mishahara ya wazee wa vijiji na ya makamishna wetu, jameni utaona haya ni mateso. Kila mara, ni lazima utapata kamishna akimwambia mzee wa kijiji atoe taarifa fulani, ilhali mzee huyu hata amelala njaa. Kwa ubinadamu, kuna umuhimu wazee hawa waangaliwe. Hawa ni binadamu kama binadamu wengine, na wako na mahitaji ya chakula, malazi na mavazi. Vile vile, hawa ni wazee ambao bila shaka wako na watoto na majukumu ya kuona kwamba watoto wao pia wamepata elimu, na wamelelewa kama watoto wengine. Kwa sababu ya haya, kuna haja sisi Wabunge wa Bunge la Kitaifa, tuunge mkono Hoja hii, na kuhimiza Serikali itekeleze Hoja hili. Wakati umefika tuweze kuwatazama kwa karibu wazee wetu. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}