GET /api/v0.1/hansard/entries/675011/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675011,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675011/?format=api",
"text_counter": 122,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Chea",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1694,
"legal_name": "Mwinga Gunga Chea",
"slug": "mwinga-gunga-chea"
},
"content": "Usalama unaweza kuenda chini kila siku kwa sababu ya kutowapa motisha wazee wa vijiji.Tukumbuke kwamba, wazee hawa wako pale chini kijijini, na bila shaka taarifa na habari zote, ziwe nzuri ama mbaya, hawa wazee wetu huwa nazo. Kwa hivyo, wale maafisa wote ambao tunawaita intelligence officers, bila shaka huwategemea sana wazee wetu. Kinachotushangaza ni kwamba hawa maofisa hupata hela nyingi lakini wazee wetu hawapati kitu. Hawa wazee wako na majukumu mengi sana. Siku nyingine, tunawaonea huruma. Utapata wakati jambo fulani limefanyika, wao huhusishwa. Kwa mfano, mtu ameuwawa na mzee wa kijiji atabidi akae pale kutoka saa nne usiku hadi saa mbili asubuhi, wakati gari la polisi litakapokuja kubeba maiti ile. Huyu ni mzee ambaye ameacha nyumba yake, majukumu yake na shughuli zake kushughulikia jambo hili. Badala ya kupoteza hela nyingi kuandaa mikutano katika hoteli za kifahari na kupeleka watu nchi za nje, ni lazima fikra zetu zote zielekezwe katika kuangalia masuala ya wazee hao. Tunaweza pata tatizo kwa serikali za kaunti kwa sababu zimeanza kuleta watu ambao wanaambatana na sheria za kaunti katika mipangilio."
}