GET /api/v0.1/hansard/entries/675606/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 675606,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/675606/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Ahsante, Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Kamati hii ya Uteuzi vile ilivyosomwa na mwenzangu ili ikaanze kufanya kazi yake haraka iwezekanavyo. Uteuzi wa Kamati hizi saa zingine unachangamoto zake. Ni ombi langu kwa Waheshimiwa wahakikishe wamebainisha ni akina nani wanaweza kuwa kwa Kamati hizi. Mara nyingi, inabidi uangalie vile utakavyosambaza wenzako katika Kamati mbalimbali. Kamati ya Ratiba za Bunge ilionelea haya majina yaletwe mbele ya Bunge hili ili Wabunge wafikirie na kuyaweka maanani, ili yaidhinishwe na uteuzi huu uweze kufanya kazi. Kwa hayo machache, Mhe. Spika, naomba kuunga mkono uteuzi wa Kamati hii."
}