GET /api/v0.1/hansard/entries/680138/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 680138,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/680138/?format=api",
"text_counter": 18,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Shukrani sana Mhe. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Nataka kuunga mkono mapendekezo katika malalamishi haya. Mwanzo, kwa sababu katika benki za kiislamu, sheria zake huwa ni za kiutu zaidi. Nakubali kuwa baadhi ya senti za Serikali hazitaharibika zikiwekwa katika benki kama hizo. Pesa za Serikali pia hazitaliwa ovyo ovyo na benki zenye kulaghai watu na benki zenye tamaa ya kula pesa za Serikali ambazo zinahitajika kutumika kwa wananchi humu nchini, ambao wana shida nyingi. Jambo lingine ambalo nakubaliana nalo ni kuweka vikwazo katika asilimia ya pesa ambazo Serikali kuu inaweza kuchukua kama mkopo kutoka benki zozote. Kiwango cha asilimia tano ya bajeti ya nchi - kama nimeelewa sawa - ni jambo nzuri sana. Hivi sasa, tunajua Serikali kuu imechukua madeni makubwa ambayo yatatulemea sisi na vizazi vijavyo. Kwa hivyo, kutunga sheria ambayo itaizuia Serikali kuu kukopa kupita kiwango fulani itakuwa jambo la busara. Ahsante."
}