GET /api/v0.1/hansard/entries/685408/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 685408,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/685408/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika. Ningependa kuchangia hili jambo muhimu ambalo limeletwa na Mhe. Sumra kuhusu Wakenya maskini wanaopelekwa hospitalini. Mgonjwa maskini akipelekwa hospitalini, madaktari wanakataa kumtibu. Jukumu la kubadilisha sheria na kuhakikisha kuwa mambo kama haya yamerekebishwa ni la hili Bunge la Kenya. Kila wakati wagonjwa wanapelekwa hospitali na wanapoaga dunia, kama alivyosema Mhe. Neto, hospitali zinakatalia miili isipelekwe nyumbani. Ningependa kusihi Kamati ya Afya ilizungumzie suala hili ili suluhu ipatikane. Asante, Mhe. Naibu Spika."
}