GET /api/v0.1/hansard/entries/717239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 717239,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/717239/?format=api",
"text_counter": 32,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante Mheshimiwa Spika kwa mjadala huu asubuhi hii na kwa kunipatia nafasi niuunge mkono. Tukiunga mkono mjadala huu, ni muhimu tukubaliane sote Wabunge kuwa tumeitwa kwa Kikao Maalum kuangalia Hoja ambazo ziko mbele yetu. Hoja ni kuangalia waliopendekezwa kuwa Mwenyekiti anayeangalia shirika linalohusika na ufisadi na hao ambao watakuwa wakiangalia mambo ya usajili na mipaka ili tuhakikishe kuwa upigaji kura utahalalishwa, na wenyewe ni watu ambao wamehalalishwa na Bunge. Hii ndio maana tumeitwa tuje Bungeni siku hii ya leo kwa Kikao Maalum. Tumeangalia yale masaa na muda ambao unaombwa Wabunge wauchukue kwa mjadala wa kwanza kuanzia 2.30 p.m. hadi 4.30 p.m., na mjadala wa pili kuanzia 4.30 p.m. hadi wakati tutaumaliza hata kama ni saa mbili usiku au zaidi ya hivyo. Ni muhimu Wabunge waje watoe hoja, maoni na mapendekezo yao waziwazi ili tukienda kwenye uchaguzi tuwe sote tumeridhika kuwa wale ambao wamependekezwa wanaweza kufanya kazi hii, na kwa niaba ya wananchi wa Kenya, watatekeleza wajibu wao. Bila shaka Wabunge watapata nafasi ya kusoma Ripoti ya Kamati ambayo imepeanwa hivi sasa ili tukija mchana, tuwe tumejua yale ambayo yamesemwa humo ndani na tunaweza kutoa maoni na mapendekezo yetu bila mapendeleo yoyote. Kwa haya machache, ninaomba niunge mkono muda ambao umependekezwa wa dakika tano kwa kila Mbunge ili apate kutoa mapendekezo yake. Ninatamatisha na kuunga mkono Hoja hii. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}