GET /api/v0.1/hansard/entries/744313/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 744313,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/744313/?format=api",
"text_counter": 919,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "vile Serikali imetumia pesa, na kama pesa zimefujwa ama zimetumika sawasawa, amefanya kazi nzuri. Mhe. Keynan na wenzake wamefanya kazi nzuri. Chuo hiki ni cha muhimu sana. Lakini juu ya hapo, ni jambo la muhimu kuwa Wakenya wafahamu kuwa haiwezekani kuwa tunajenga chuo miaka nenda miaka rudi na hakiishi. Kama chuo kilichorwa na mipangilio ilikuwa kuwa awamu ya kwanza ijengwe kwa kutumia pesa taslimu karibu bilioni mbili, basi wangekuwa wamemalizia awamu hiyo ya kwanza. Halafu, kama kuna chochote cha kuongezewa, kiongezewe baadaye. Lakini kwa sasa hivi, miaka imesonga mbele. Hata reli kutoka Mombasa hadi Nairobi ilijengwa kwa miaka mitatu. Ulimwengu mzima, tunapongezwa kuwa hakuna pahali pengine reli inajengwa kwa kasi namna hiyo. Chuo hiki kingekuwa kinawafaa watoto wetu hapa nchini Kenya, na haswa sisi wapwani ambao swala la utalii ni la muhimu sana kwetu na Wakenya wote kwa jumla. Mpaka sana, watu wanakizungumzia kuwa kimetumia pesa mara tano ya kiasi kile ambacho kilikuwa kimetarajiwa kutumika. Na hata leo tunavyozungumza, chuo bado hakijakamilika. Ni mambo ya kustaajabisha sana. Ni lazima ufujaji wa pesa Kenya hii ukome. Katika uchaguzi unaokuja, wananchi watafanya uamuzi kuwa ufujaji wa pesa lazima ukome. Katika hali ya ugatuzi, vyombo vya ugatuzi na kazi za ugatuzi, unaona kuwa ufujaji unaendelea. Tunaomba kuwa Wakenya wafanye uamuzi, wachague viongozi ambao wataweza kutumia pesa vizuri na vile vile chuo hiki kiweze kukamilika. Mhe. Rais anataka chuo hiki kikamilike maanake anajua faida na hali ya uchumi ambapo utalii unasaidia. Tunaomba chuo hiki kimalizike mara moja. Lakini juu ya hapo, ufujaji wa pesa lazima uchungwe na ulindwe ili chuo hiki kiweze kutekeleza matarajio ambayo kilitarajio kutekeleza. Nikimalizia, nawaunga mkono wenzangu kwa yote waliyosema na kwa wote waliotoa mapendekezo. Tunaomba chuo hiki kikamilike."
}