GET /api/v0.1/hansard/entries/766992/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 766992,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/766992/?format=api",
    "text_counter": 1597,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. King’ara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia mwanya wa kuweza kuunga mkono mjadala huu ulio na uzito mkuu katika Kenya yetu tupendayo. Kenya inasemekana kuwa ni eneo la ukulima. Lakini ukiangalia orodha ya madini yaliyo katika Kenya yetu, ni mengi kuliko ule ukulima tunafanya. Ukianzia na theluji, petroli ambayo imepatikana juzi, dhahabu iko, titanium iko, hewa ya uwekezaji na vile vile mvuke katika eneo la Bonde la Ufa umechangia pakubwa sana kwa umeme. Ombi langu ni wakati tunajaribu kujadili na kutilia uzito mikakati hii mwafaka itakayotumika katika Kenya yetu mpya, ni vizuri vile vile tuzingatie uzito wa uchimbaji wa madini kama jambo kubwa la kuleta mapato katika Kenya yetu. Maeneo au nchi zile zimeendelea zaidi ni zile zimetilia uzito katika uchimbaji wa madini kama petroli. Ukiangalia upande wa uarabu, utakuta hawana chochote kingine ila madini, na yameweza kutumika na kufanya maeneo hayo yatambulike duniani kote. Lakini la muhimu, hata kama tutatia uzito katika sekta ya uchimbaji wa madini, ningeomba vile vile wapangaji waangalie kiini hasa kile kinachangia sababu ya watu wanaoishi pahali kuna madini mengi, kuwa wanyonge sana. Ndio tusije tukaingia katika hilo shimo. Tutengeneze mjadala wetu na The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}