GET /api/v0.1/hansard/entries/805978/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 805978,
"url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/805978/?format=api",
"text_counter": 41,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Nataka kujumuika na wenzangu kutuma risala zangu za rambirambi kwa familia ya Sen. Okello pamoja na watu wa Kaunti ya Migori. Yeye ni mtu ambaye alikuwa amechaguliwa pale na aliyejitolea kuwafanyia wananchi kazi. Tutaungana na watu wa Kaunti ya Migori na kushirikiana nao wakati huu mgumu. Hili ni pigo kubwa sana. Hili linapaswa kuwa funzo kwetu kuhusu huu ugonjwa wa saratani. Ugonjwa huu umekuwa changamoto na kizungumkuti kwa kuwa kila wakati unawaangamiza Wakenya. Baada ya miaka 50 ya Uhuru, bado tuko pale pale kana kwamba tunachechemea. Wakenya wengi wanasafiri kutafuta matibabu katika nchi za Ulaya, India na pahali pengine wakitafuta tiba ya huo ugonjwa. Hata wakati huu tunapoomboleza mwendaa zake, Sen. Okello, linapaswa liwe funzo kwetu viongozi na Serikalli. Tuseme ya kwamba yeye awe kama funzo kwetu ili Wakenya waache kupoteza maisha yao. Hii ni kwa sababu pesa nyingi zinatumika watu wakijaribu kupigana na ugonjwa huu. Ninajua ya kwamba yuko mwenzangu pale katika Bunge la Taifa ambaye ameleta mswada wakusema kuwa saratani ifanywe janga la kitaifa. Mimi nina kubaliana naye mia kwa mia ili tuweze kujikakamua. Nina imani ya kwamba tukifanya namna hiyo Kenya itakuwa nchi nzuri ya kuishi. Naungana na watu wa Kaunti ya Migori kuleta risala zangu na za watu wa Kaunti ya Laikipia. Tutaungana na familia hiyo na watu wa Kaunti ya Migori leo na mpaka wakati wamwisho wa kumpumzisha mwenda zake, Sen. Okello.AsanteBw. Spika."
}