GET /api/v0.1/hansard/entries/806080/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 806080,
    "url": "http://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/806080/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ujenzi wa taifa. Lakini haikuwa hiyvo. Sisi pamoja na familia yake tulimpenda zaidi lakini Mwenyenzi Mungu ana mipango yake kwa kila mwanadamu. Bw. Naibu Spika, ni jambo la kusikitisha kumpoteza baba aliyetegemewa na kila mtu. Nilipokuwa hospitalini, nilijua ya kwamba yeye ndiye aliyekuwa anategemewa na familia yake. Bibi yake hana kazi na watoto hawana majukumu au kazi. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu wamepigwa na pigo kubwa katika familia. Hayo hayakuwa matarajio ya watoto wake ambao wengine wako katika vyuo vikuu. Ninatuma rambirambi zangu kwa familia. Vile vile, hatukuweza kupata nafasi ya kuona ujasiri wake hapa ndani ya Bunge la Seneti. Nayakumbuka maneno mazito aliyoyasema Prof. (Gov.) Anyang’-Nyong’o ambaye alikuwa Seneta wa Jamhuri ya Kenya lakini hivi sasa, yeye ni Gavana wa Kisumu. Aliugua maradhi haya lakini aliyatibu kwa sababu yalitambuliwa mapewa. Lakini, yeye alikuwa na bahati kwa sababu alikuwa Waziri wa Afya na alikuwa na nafasi ya kwenda kutafuta matibabu na kuweza kujua ugonjwa wa saratani umefika awamu gani. Ni wagapi watapata bahati kama yake na kuweza kutibu ugonjwa huu mara moja? Bw. Naibu Spika, ni jukumu la Serikali kutafuta mipango mwafaka kuhakikisha kwamba watu wamepimwa ili wajue kama wanasaratani badala ya kusubiri na kuanza kutibu wakati ugongwa umeenda mbali kama inavyofanyika katika nchi za ulaya. Afrika Kusini pia wanakagua watu wao ili kutambua kama wanaugonjwa wa saratani nakutafuta kinga za kuzuia ugonjwa huu. Kuna umuhimu wa Serikali yetu kuchukua nafasi hiyo ili watu wasitibiwe na mwishowe kufa. Ni heri tutumie pesa nyingi kununua vifaa ambavyo vinaweza kulinda ugonjwa huu usiingie kwenye mwili ama upatikane mapema hili uweze kutibiwa haraka. Watalaam wanasema ugonjwa huu una na awamu ya kwanza, ya pili, ya tatu na ya nne kama alivyosema Sen. (Prof.) Ongeri. Mtu akiupata katika awamu ya tano atakuwa anakaribia kufa na hakuna dawa zozote zitakazomfaa. Ni jukumu la Serikali kuhakikisha kwamba imechukuwa mipango---"
}